Mwezeshaji-Emanuel Bulendu kwa ufupi alizungumzia Mapungufu yaliyopo katika hali ya habari Zanzibar, Kinga za wabunge v/s wandishi wa habari, Maslahi ya wandishi wa habari Tanzania na Nguvu ya Vyama vya Habari katika kulinda maslahi ya wanahabari.
Mwezeshaji-Dennis Mpagaze kwa upande wake masuala yaliyochomoza ni pamoja na Tuhuma kwa wanahabari kujikita kuandika habari za watu wenye pesa na kuwatelekeza walalahoi wa taifa hili, Vyombo vya habari kutumika kuharibu maadili pia wanajamii wanachangia kiasi gani kuwezesha sekta ya habari kukabiliana na changamoto.
Mwezeshaji-Ray Naluyaga, Huwezi kuwa na jamii iliyo na demokrasia ya kweli bila kuwa na mabadiliko katika sheria, Wandishi wajikite kujiendeleza kielimu ili Media ifanye kazi yake vizuri kama inavyohitajika.
Mwakilishi wa taasisi za dini Christopher Kubeja
"Mswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba haujabainisha muda wa mtiririko mzima wa zoezi hili. Inapendekezwa ukomo wa muda uwekwe kwenye mtiririko wa mchakato wa kukusanya maoni ili kuepuka kuwa na mchakato kwa muda usiojulikana na kuleta uwajibikaji. Sambamba na hilo, kuna haja ya kuelekeza nguvu kazi pamoja na rasimali za kutosha kwenye hatua zote za mchakato ili Katiba inayoridhisha wananchi ipatikane". Maelezo zaidi tembelea
http://www.kas.de/wf/doc/kas_5088-1442-1-30.pdf?111114113050
Mwenyekiti Jimmy Luhende akitoa ufafanuzi kwa moja ya ajenda mkutanoni.
Pamoja na kujadili kuhusu "Katiba mpya na Habari" pia mkutano huo ulikaa na kujadili Mapitio ya Mkutano uliopita na marekebisho ya Katiba ya MPC.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.