Katika kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu nchini Kenya, timu ya soka ya Gor Mahia leo imetambulisha wachezaji wake sita wapya iliyosajili kwaajili ya msimu mpya unaotazamiwa kuanza wiki chache zijazo akiwemo golikipa wa zamani wa Tanzania (Taifa Stars) Ivo Mapunda.Mshambuliaji George Midenyo (pichani)amenyakuliwa na Gor Mahia toka timu ya Tusker ya nchini humo, Ivo Mapunda na mwenzake Rama Salim wamesajiliwa kutoka Congo United, wengine ni Yusuf Juma kutoka Thika United, Ali Hassan na Hugo Nzoka toka Sony Sugar.
Gor Mahia safari hii imejizatiti kufukuzia hatimaye kuyanyakuwa mataji yote matatu nchini humo likiwemo kombe la ligi kuu ya KPL, KFK Cup na KPL Top 8 trophy.
”Rasmi Soko Kuu la Manispaa ya Bukoba lavunjwa”
-
Soko Kuu la Manispaa Bukoba limevunjwa ili kupisha ujenzi wa soko jipya la
kimataifa unaotarajiwa kuanza muda wowote.
Kwa Wakati tofauti wameonekana Wafa...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.