

Bwana Zuma alisema leo ni siku ya furaha kwa watu wa Afrika Kusini, ambao waliangamiza ukoloni na ubaguzi wa rangi, kwa kusaidiwa na Afrika na ulimwengu.

Bwana Nelson Mandela hakuweza kuhudhuria kwa sababu ni dhaifu.



Kati ya wageni waliohudhuria sherehe hizo ni Kasisi Jesse Jackson, mwanaharakati maarufu wa Marekani wa kutetea haki za weusi.

Alisema: "Baada ya karne moja kutoka ma- dhalilisho kachomoza Nelson Mandela, Thabo Mbeki, Jacob Zuma, na Barack Obama. Ni karne ya mifano ya kuvuka vizingiti vikubwa.
Na hofu waliyokuwa nayo wazungu - kwamba weusi watalipiza kisasi - hayakutokea hayo".
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.