ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 23, 2011

WIZARA YA ARDHI YAIBWAGA KAHAMA MINING Ltd.


Na:ANNA MASSAO

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeshinda kesi yake dhidi ya kampuni ya uwekezaji ya kigeni ya Kahama Mining Corporation Ltd. kuhusu eneo la kiwanja kilichopo eneo la Oysterbay.

Hayo yalisemwa jana na Prof. Anna Tibaijuka, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi katika mkutano wake na waandishi wa habari ambapo ulifanyika ukumbi wa habari Maelezo jijini Dar- es- Salaam. waziri huyo pia aliongozana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Patrick Rutabanzibwa, Mkurugenzi wa Mipango miji, kamishna wa Ardhi na Mwanasheria wa wizara hiyo.

Prof. Tibaijuka aliongeza kuwa baada ya uamuzi wa mahakama kuitaka wizara yake kurudisha kiwanja ambacho kwa sasa kimejengwa shule ya Sekondari ya Bongoyo waliamua kukata rufaa ambapo walishinda kesi hiyo, akizungumzia suala hilo pia Katibu Mkuu Patrick Rutabanzibwa alisema, ‘’ Tunaishukuru mahakama ya rufaa kwasababu imetenda haki kwa manufaa ya Watanzania”

Chanzo cha mgogoro huo ni baada ya kampuni hiyo ya kigeni kumilikishwa ardhi na Halmashauri ya wilaya Kinondoni ikishirikiana na Oysterbay Properties Ltd. bila kuishirikisha wizara husika ambayo baadae ilitoa kibali cha kujengwa kwa shule hiyo ya sekondari na kampuni hiyo kuamua kuishtaki baada ya kukataa eneo lingine la wazi walilopewa.

Profesa pia aliongoza zoezi la kuweka mabango eneo la Sinza ili kuonesha wananchi kuwa maeneo hayo ni ya wazi na hayastahili kuuzwa wala kujengwa na kuwataka wananchi wanaoishi kwenye maeneo ya wazi kuhama katika maeneo hayo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.