ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 29, 2011

LOWASSA AIBUKA KAMA ZUMA

HARAMBEE zote alizopata kusimamia ndani ya jamii zimetoa matunda mfano hii ya Kanisa Katoliki Mwanza.

WAZIRI mkuu mstaafu Edward Lowassa hivi majuzi ametoa utetezi tosha kwenye Halmashauri Kuu ya CCM kwa staili inayoweza kufananishwa na ile ya Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini alivyojisafisha na tuhuma zilizokuwa zikimkabili ndanio ya chamachake cha ANC kabla ya kuzipangua na kuibuka shujaa hadi kuja kuwa mkuu wa nchi.

Katika utetezi huo wa hivi majuzi mjini Dodoma, Bw. Lowassa alionyesha kuwa yeye si mtu fisadi kama ilivyokuwa inaelezwa na baadhi ya viongozi waandamizi wa chama hicho tawala kiasi cha kumfanya aonekane kuwa si kiongozi safi mbele ya jamii.

Utetezi huo ambao umemgusa hata Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Rais Jakaya Kikwete mwenyewe unaonekana kuizika rasmi hoja ya “Kujivua Gamba” ndani ya chama hicho iliyokuwa awali imelengwa kwa Bw. Lowassa mwenyewe pamoja na Mbunge wa zamani wa Igunga Bw. Rostam Aziz na Mbunge wa Bariadi Magharibi Bw. Andrew Chenge.

Katika uteuzi huo akielekeza hoja zake Rais Kikwete, Mbunge huyo wa Monduli alisema baadhi ya viongozi ndani ya chama wamekuwa wakimhusisha na tuhuma za ufisadi kupitia mkataba wa Richmond wakati Rais akijua kwamba hakuna jambo alililifanya ambalo hakulifanya au ambalo hakumtuma yeye (Kikwete).

Bw. Lowassa ambaye katika utetezi wake alikuwa ameshika mkono Hansard ya Bunge, alisema ripoti ya kamati Teule ya Bunge ambayo ilisababisha ajiuzulu uwaziri mkuu Februari mwaka 2008 alisema bayana kwamba alifikia hatua hiyo kutokana na makosa ya watendaji wa chini yake.

Mbali ya hayo Bw. Lowassa alirejea kauli za Rais Kikwete mwenye we ndani ya vikao vilivyopita vya NEC ambapo alipata kukaririwa zaidi ya mara moja akisema kwamba hakukuwa na ushahidi wa rushwa katika mkataba wa kampuni ya kufua umeme ya Richmond.

Bw. Lowassa aligusia pia matamshi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda bungeni ambayo yalithibitisha kutokuwepo kwa rusha katika mchakato huo wa zabuni na pia alikumbusha historia ya neno Ufisadi akisema lililetwa na CHADEMA kupitia mkutano wa hadhara wa Mwembeyanga ambapo viongozi 11 wa CCM walitajwa kwa ufisadi akiwemo yeye.

Alisema ni jambo la ajabu kwamba viongozi wa CCM walilidaka neno hilo na kuanza kulitumia kuwashambulia wenzao akiwemo yeye, katika mambo ambayo hayakuwa na ukweli.

Lowassa pia alihoji Katibu Mwenezi wa Taifa wa CCM Bw. Nape Mnauye anapata wapi uhalali wa kimaadili wa kumtuhumu yeye kwa ufisadi hata kufikia kudai kwamba amekipotezea heshima chama hicho wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Akifafanua, alisema matokeo ya kura alizopata Rais na yeye mwenyewe katika Jimbo la Monduli yanazidi asilimia 89 na kwamba wakati yeye (Lowassa) na wengine wakipigania chama chao kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu, Bw. Nape na baadhi ya wanasiasa wengine wanaomshambulia walikuwa katika harakati za kusajili chama cha jamii (CCJ)
Akirejea tuhuma dhidi yake ambazo alisema hazina ushahidi, huku akitumia neno la Kiingereza “perception”, Bw. Lowassa alikumbusha Rais Kikwete jinsi yeye (Kikwete) alivyozushiwa tuhuma za ukosefu wa maadili na mwnasiasa mkongwe Bw. Paul Sonzigwa mwaka 2003.

Bw. Lowassa alisema tuhuma hizo dhidi ya Kikwete ambaoz ziliwasilishwa mbele ya kikao na Bw. Sonzigwa kwa niaba ya Kamati ya maadili ya CCM, zilizimwa kwa hekima ya Mwenyekiti wa Taifa wa CCM wa wakati huo Rais mstaafu Benjamin Mkapa, wakati ule, leo asingekuwa amekaa katika kiti hicho, huku akisisitiza kuwa ni makosa kuwahukumu watu pasipo ushahidi.

Alisema kama kungekuwa na makosa aliyotenda, kanuni za CCM ziko wazi na zisingefuatwa, ikiwa ni pamoja na kuitwa katika kamati ya Maadili ya chama ambako angehijiwa juu ya tuhuma hizo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.