Kanali Gaddafi ameapa atapigana mpaka kufa, ingawa amepoteza sehemu kubwa ya udhibiti wake nchini Libya.
Nato, ambayo imekuwa ikiendesha harakati za kijeshi za anga kuunga mkono Maamuzi ya Umoja wa Mataifa kuwalinda ria wa Libya, imekataa kusema chochote katika ripoti yake.
Msafara huo wenye silaha umevuka mpaka na kuingia Niger na kufika mji wa Agadez Jumatatu, taarifa za kijeshi kutoka Ufaransa na Niger zimelifikia Shirika la Habari la Reuters.
Wamesema msafara huo una magari kati ya 200 na 250 na unasindikizwa na jeshi la Niger. Wasemaji kutoka Agadez wameiambia BBC kuwa kati ya magari hayo 200, 60 ni ya Libya na yaliyosalia ni kutoka Niger.
Baadaye afisa mmoja kutoka Baraz la Mpito la Taifa Libya (NTC) aliliambia Shirka la Habari la Reuters kuwa msafara huo umebeba dhahabu na fedha na umevuka kuingia Niger kutoka katika mji unaoshikiliwa na Gaddafi wa Jufra.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.