Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akimkabidhi fedha Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Issa Shaaban bin Simba kiasi cha sh. milioni 13, kwa ajili ya kusaidia shule ya sekondari ya Edward Lowassa iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Mufti ambaye ni mlezi wa shule hiyo, Shule hiyo inatarajiwa kufunguliwa rasmi mwakani kwa kuanzia na wanafunzi 200 wa kidato cha kwanza, na kwamba fedha hizo zitatumika kukamilisha baadhi ya mambo ya shule hiyo ikiwemo kujenga bweni la watoto 30, choo cha shule, kisima cha maji na shule itajihusisha zaidi kusomesha yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Kulia ni aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana ambaye pia ni mlezi wa shule hiyo.
MKUU WA MKOA SINGIDA AIPONGEZA TASAC
-
MKUU wa Mkoa wa Singida Mhe. Halima Dendego amelipongeza Shirika la
Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa utekelezaji wa majukumu yake ya
kuhakikis...
Picha za kipekee za mazishi ya Papa Francis
-
Umati mkubwa ulikusanyika katika Jiji la Vatican tangu asubuhi kwa ajili ya
mazishi ya Papa Francis, yaliyohudhuriwa na viongozi karibu kutoka kote
duniani
”Rasmi Soko Kuu la Manispaa ya Bukoba lavunjwa”
-
Soko Kuu la Manispaa Bukoba limevunjwa ili kupisha ujenzi wa soko jipya la
kimataifa unaotarajiwa kuanza muda wowote.
Kwa Wakati tofauti wameonekana Wafa...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.