MICHEZO ILIYOTIA FORA, KUSISIMUA NA KUWA KIVUTIO KWA WENGI LEO KATIKA UFUNGUZI VIWANJA VYA BWIRU BOYS SEC SCHOOL. Katika mchezo wa Riadha kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi (albino) matokeo kwa mita 100 wavulana yalikuwa ni Joseph John wa Shule ya msingi Mitindo wilayani misungwi aliyenyakuwa nafasi ya kwanza nayo ya pili ikinyakuliwa na Fadhili Michael wakionekana pichani.
Riadha kwa walemavu wasioona wavulana ushindi wa kwanza umenyakuliwa naye John Robert (kulia jezi rangi ya samawati) aliyetumia sekunde 13.29 huku nafasi ya pili ikichukuliwa na James Emmanuel aliyetumia muda wa sekunde 14.37 .
Riadha kwa walemavu wasioona wasichana Swisbat Kabele akiifikia kingo na kuwa mshindi kwa kutumia muda wa sekunde 17.29 akifuatiwa na mshindi wa pili Mbalu Athuman aliyetumia muda wa sekunde 17.79.
Ma-Time watcher wakiwa bize kuhakiki washindi wa michuano hiyo.
1.Mashindano ya mwaka huu 2011 yanashirikisha michezo ifuatayo ambayo ni
2.Mpira wa miguu – Wavulana pekee
3.Mpira wa miguu kwa wenye ulemavu - wasichana
4.Netibali wasichana
5.Mpira wa wavu – wasichana kwa wavulana
6.Riadha wote
7.Riadha kwa walemavu
8.Taaluma kwa masomo ya Hisabati, Kiswahili, Hati, Huji (Historia, Uraia na Jiografia) na Kiingereza.
Lengo la mashindano hayo ni kutumika kama njia ya kupata wachezaji watakaoshiriki michuano ngazi ya Kitaifa sambamba na kuwasaka wenye vipaji maalum na kupunguza idadi ya siku za mashindano na wachezaji kwa ngazi ya taifa hivyo kupunguza gharama ya uendeshaji na kuwezesha mashindano kufanyika ndani ya kipindi cha likizo kubwa. Mashindano ya kitaifa yatafanyika tarehe 25/06/2011 hadi tarehe 07/07/2011 kwenye kituo cha Kibaha – Pwani. Timu zitakazoshiriki ni za kikanda ambapo zitakuwepo jumla ya kanda 11.
Mgeni rasmi kwa ufunguzi wa mashindano hayo mkoani Mwanza hii leo alikuwa Mama Getrude Kulindwa katibu maidizi huduma za jamii, ambaye aliambatana na afisa elimu wa mkoa Ramadhani Chomola.
Engo ya wanamichezo.
Engo nyingine.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.