ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 13, 2011

HATIMAYE WANJIRU-BINGWA WA OLIMPIKI ALIYEFARIKI MWEZI ULIOPITA AZIKWA.

Maelfu ya watu wamejitokeza katika mazishi ya aliyekuwa bingwa wa michezo ya Olimpiki mbio za marathon raia wa Kenya Sammy Wanjiru juzi Jumamosi aliyefariki mwezi uliopita baada ya kuanguka kutoka kwenye ushoroba wa nyumba yake. Mazishi yalifanyika katika kijiji cha Heshima, eneo la Ol joroonok na kuongozwa na mjane wa Marehemu Trizah Njeri.Katika hali isiyokuwa ya kawaida mama mzazi wa wanjiru alitinga nyumbani kwa Marehemu akiwa na panga alilolificha kwenye mfuko akidai kuwa atamkata nalo mtu yoyote anayeunga mkono mazishi hayo.

Mjane wa Marehemu Trizah Njeri-pichani akiweka shada la maua.
Hata hivyo mazishi yalifanyika katika uwanja wa michezo katika wilaya alikozaliwa, Nyahururu, katika jimbo la Rift Valley, huko Kenya chini ya ulinzi mkali wa polisi. Mahakama iliamuru wiki hii kuwa Wanjiru, aliyekuwa na umri wa miaka 24, anaweza kuzikwa licha ya kuwa uchunguzi unaendelea kuhusu mazingira yaliyosababisha kifo chake na kusema kuwa Wanjirua likufa ama katika ajali, au alijiua baada ya mkewe kumfumania na mwanamke nwengine.

Mama mzazi wa mwanamichezo huyo alisusia mazishi na Katika kile kinachoonyesha kupata heshima ya kitaifa alipigiwa saluti ya mizinga 21 wakati jeneza lake lilipoteremshwa kaburini katika shamba lake.


Wanjiru enzi zake mchezoni:
Wanjiru alikuwa Mkenya wa kwanza kushinda medali ya dhahabu ya Olimpiki katika mbio za marathon za michezo ya Beijing mnamo mwaka 2008 na akihesabiwa kuwa mojawapo wa vijana chipukizi hodari.Mazishi yake yalihudhuriwa na wanariadha mashuhuri wa Kenya na watu mashuhuri.

Picha na habari kwa hisani ya Mirindimo

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.