Meneja wa timu ya mkoa wa Mara, Chiganga Pascal (shoto) akipokea vifaa toka kwa Mwenyekiti wa chama cha soka mkoani Mwanza Jackson Songora, tayari kwa kuianza ligi ya Kili Taifa Cup 2011, makabidhiano yaliyofanyika leo katika ofisi za uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Jackson Songora akizungumza wakati wa sherehe za kukabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa ajili ya Mashindano ya Kili Taifa Cup yanayoanza kesho katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Jumla ya timu nne za kituo hiki chenye timu toka mkoa wa Kagera, Mara, Shinyanga na Mwanza zimekabidhiwa vifaa hivyo tayari kushiriki michuano hiyo inayotaraji kuanza kutimua vumbi kuanzia kesho katika vituo vyote nchini.
(Picha na Mohamed Mambo)
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.