ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 14, 2011

SPRITE YAPANIA KUINUA KIKAPU MKOANI MWANZA

Chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Mwanza (MRBA) kwa kushirikiana na kampuni ya Nyanza Bottling kupitia kinywaji chake cha sprite kiliandaa bonanza la 3 on 3 spriteball lililofanyka katika uwanja wa mpira wa kikapu uliopo ktk chuo kikuu St. Augutine Mwanza (SAUT) siku ya jumamosi ya tarehe 12/03/2011Jumla ya timu 16 zilishiriki bonanza hili kwa kuanza ktk mtindo wa ligi za makundi 4 yenye timu 4 kila kundi na baadae timu moja kutoka kila kundi ziliingia katika hatua yua nusu fainali na kisha fainali. Pia kulikuwa na mashindano ya kudank na kushoot (Dunking competition & Shooting Competition)

Kwa upande wa Dunking Competition Erick John kutoka Bugando Worrious aliibuka mshindi baada ya kuwashinda Timothy Ngalula (Fire) na Moses Jackson (Worrious) hapa akiruka toka mstari wa free throw aka mstari wa penati.

Erick John bingwa wa kudank. Bugando Heat ilichukua ubingwa kwa kuifunga timu ya Bugando fire katika hatua ya fainali na kutunukiwa kikombe pamoja na mipira 2 huku bugando fire wakipata mipira 2.

Moses Jackson huyooo angani! Timu za SAUT na Bugando Worrious ilipata mpira mmoja mmoja baada kufika hatua ya nusu fainali, pamoja na hao timu za Saut B, Young Saut, Dolphin Pasiansi na St. francis walipata mpira mmoja mmoja kila timu baada ya kushika nafasi ya pili kutoka kila kundi.

Nae mgeni rasmi Mr. Mussa mziya amekipongeza chama mpira wa kikapu mkoa kwa juhudi zao za kuweza kuendesha mashindano mbalimbali hapa mkoani ukizingatia kuwa Mwanza ni kitovu cha wachezaji wenye vipaji ambao wamekuwa wakionekana katika mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kwani ukizatia pia Hasheem Thabeet ni mtu kutoka hapa hapa Mwanza. Pia ameiomba kampuni ya nyanza bottling kuendelea kusaidia mchezo huu hasa program kwa vijana ili waweze kuinua vipaji vyao.

Ben Mwangi akifuatilia game kwa umakiiiini..

Mabingwa Heat pamoja na viongozi toka Nyanza Botling Company, MRBA na Mgeni rasmi.

Akizungumza kwa niaba ya chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Mwanza (MRBA), Kizito Sosho Bahati alitoa shukrani za chama kwa kampuni ya nyanza bottling kwa kudhamini mashindano haya na kuwaomba kuendelea kudhamini mashindano haya na pia kuiomba kampuni kuisaidia timu ya jiji la Mwanza (Rocky City Team) inayotarajia kwenda kushiriki mashindano ya majiji ya Afrika Mashariki na Kati jijini Nairobi nchini Kenya.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.