Katika kujiandaa na mchezo huo Kampuni ya Ulinzi jijini Mwanza ambayo pia ni moja kati ya wadhamini wa Blogu hii VSS Security Group kwa kushirikiana na club maarufu jijini Mwanza STONE CLUB jana jioni wamemwaga Ma-Full seti ya vifaa vya michezo Jezi jozi mbili, Shin guard, Sox na Viatu kwa timu ya Watangazaji na MaDJ wa Mwanza.
Kiingilio kwa mchezo huo ni shilingi 2,000/= mzunguko na 3,000/= jukwaa kuu. Burudani ya muziki wa bongo fleva kutawala jukwaani kuanzia saa 6 mchana kabla ya mchezo.
M 2tha P ambaye ni msemaji wa Bongo Fleva FC amesema kwamba timu hiyo itakuwa jijini Mwanza kwa mechi moja na timu itaambatana na nyota wake ili kulipendezesha pambano lao. Wachezaji ambao watasafiri na timu ni pamoja na Ngwear, Ben Kinyaiya, H-Baba, Soggy Doggy, Suma G, Richie One, Insepecta Haroun na Q Jay. Wengine ni KR Mullah, Z Anto, Godi Mwokozi, Kalapina, Mansu Li na yeye mwenyewe M 2tha P.USIKOSE JUMAMOSI HII....CCM KIRUMBA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment