Sasa wakazi wa kanda ya ziwa wamepata tiba ya kiu ya burudani kwa ujio wa bendi mpya inayoitwa 'HILL WAY' ni bendi inayoundwa na vijana waliobobea katika mafunzo ya muziki sambamba na uzoefu kwa kupiga katika bendi mbalimbali hapa nchini na Kongo.Mpiga gitaa la besi Abineli akionesha ujuzi wake mbele ya kamera ya Clouds tv.
Ni ndani ya kipindi kifupi tu takribani miezi 3, bendi hii imewakamata wapenzi wa muziki wa dansi Mwanza na kuziba pengo la wakazi wa mji huu kukosa burudani ya muziki wa dansi wa kisasa levo za Akudo, Fm, Twanga na kadhalika.
Bendi hii yenye vijana waliona hamu ya mapinduzi katika tasnia ya burudani inamwaga raha katika viunga vya Hill way pub, MJ pub na kushughulika na mialiko mbalimbali.
IJUMAA HII WANAPIGA PALE MJ PUB KONA YA BWIRU NENDA UKAWAONE! SOON NTAKULETEA KIKOSI KAMILI.
RAIS SAMIA AFTURISHA WATOTO KIKOMBO DODOMA
-
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.
Mwanaidi Ali Khamis akigawa iftar kwa mmoja ya mtoto anayelelewa katka
Makao ...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.