Nganyanga alisema aliona kundi la watu wakiwa wamekimbilia kupumzika kwenye baraza la nyumba hiyo baada ya kukimbia nyumba zao, wakati wakiwa katika maombi ya kuomba Mungu awaepueshe na janga hilo, ghafla aliona vumbi likitimka kwenye nyumba hiyo.
Mwenye nyumba hiyo, Farida Magwa, ambaye alikuwa akibubujikwa na machozi alisema akiwa barabarani na familia yake, aliambiwa kuwa nyumba yake imepigwa bomu na kuna watu wameuawa. Alisema baadaye waliweza kutoa maiti za watu watano, wakiwamo watoto wawili, lakini kuna uwezekano wa wengine bado wapo wamefunikwa na kifusi cha ukuta huo.
Habari zaidi zinasema mamia ya wananchi wameyakimbia makazi yao. Mamia ya watu kutoka Gongolamboto, Karakata, Tabata, Segerea, Ukonga, Kitunda, Banana na maeneo mengine jirani, wameonekana wakipanda daladala, wengine wakining'inia nyuma ya magari hayo yaliyokuwa yakielekea katikati ya jiji, huku mamia kwa mamia ya watu walikuwa wakitembea kwa miguu kuokoa maisha yao.
Ni hii mara ya pili kwa milipuko kama hiyo kutoka jijini Dar es Saalam katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, mwaka wa 2009 zaidi ya watu ishirini waliuawa na wengine 300 kujerihiwa.
kwa picha zaidi tenbelea MICHUZI.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.