Ankara hizo ambazo ni siri kati ya mteja na MWAUWASA zimeonekana kufunga vifurushi vya bidhaa kama chumvi, sabuni, vitafunwa, misumari, na bidhaa ndogondogo. Pepa hizo za Ankara zinauzwa kwa anayehitaji ambapo furushi moja linauzwa kwa shilingi mia tatu.
Maafisa husika toka MWAUWASA wanasema kuwa kwa kawaida Ankara hizo hupelekwa posta ili ziwafikie wateja wake kupitia masanduku huduma ambayo ilisitishwa rasmi Mei 2010 baada ya wateja kubainika kuwa hawachukui Ankara hizo na wengine masanduku kunyang’anywa bila taarifa kwenda mamlaka ya maji. “inawezekana watumishi wa Posta wasio waaminifu wanazichukuwa Ankara hizo na kuziuza kwa wamiliki wa maduka, lakini tutathibitisha baada ya uchunguzi kufanyika”
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.