Rais anayetetea kiti chake Laurent Gbagbo amekula kiapo cha kuongoza muhula mpya, lakini saa kadhaa baadaye Alassane Ouattara pia akala kiapo.
Marekani, Umoja wa Mataifa na Ufaransa zimesema Bw Ouattara ndiye ameshinda uchaguzi huo. Bw Ouattara alitanagzwa mshindi la Tume ya Uchaguzi, lakini matokeo hayo yalitenguliwa na Baraza la Katiba, ambalo linaongozwa na mshirika wa Bw Gbagbo.
Uchaguzi wa raindi ya pili ya urais, ulikuwa na lengo la kuliunganisha taifa hilo ambalo ndio mzalishaji mkubwa zaidi ya kakao duniani, baada ua kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2002.
Watu wasiopungua wanne wamekufa kuhusiana na ghasia za uchaguzi wiki hii, katika mji wa Abidjan.
Mitaani wafuasi wa upinzani wanaandamana wakipinga hatua ya Bw Gbagbo, wakisema hayo ni mapinduzi. Wafuasi wa Bw Gbagbo wanasisitiza kuwa Umoja wa Mataifa hauna haki ya kusema nani ni mshindi, na wametishia kuwafukuza wafanyakazi wapataoo 8,000 wa umoja huo.
KWA HISANI YA bbc swahili.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.