BAADA YA KUZINDULIWA MICHUANO YA LIGI SOKA YA (DUME CUP) MKOANI MWANZA TIMU KUMI NA SITA ZA MADEREVA NA WAPIGA DEBE ZA VIJANA WENYE UMRI WA MIAKA KUMI NA TANO HADI AROBAINI NA TANO ZIMEANZA KUJIHAMI KUTWAA UBINGWA WA LIGI HIYO.
KATIKA MCHEZO WA UFUNGUZI AMBAO UMEFANYIKA KWENYE UWANJA WA MABATINI, KIKOSI CHA TIMU YA SOKA YA MASKANI FRESH KIMEFANIKIWA KUTOA DOZI YA KICHAPO CHA MABAO 5 KWA 4 DHIDI YA KIKOSI CHA TIMU YA SOKA YA MWANZA COMPLEX.
LENGO LA LIGI HIYO NI KUWAELIMISHA VIJANA KUHUSU NAMNA NA KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI. BAADA YA MICHUANO HIYO KUZINDULIWA MADEREVA NA WAPIGA DEBE MKOANI HAPA WATABADILIKA NA KUCHUKUA TAHADHARI YA NAMNA YA KUEPUKA MAAMBUKIZI MAPYA YA VIRUSI VYA UKIMWI KUTOKANA NA ELIMU INAYOKWENDA SAMBAMBA NA MICHUANO HIYO.
ZAWADI KWA MSHINDI WA KWANZA NI NG’OMBE DUME NA KOMBE, WA PILI NI KOMBE NA MBUZI, WA TATU NI KOMBE PEKEE HUKU WASHIRIKI WALIOSALIA KUPATA ZAWADI MBALIMBALI ZA KIFUTA JASHO ZIKIWEMO TISHETI ZENYE UJUMBE HUSIKA KAMA SHUKRANI YA USHIRIKI.
RAIS SAMIA AFTURISHA WATOTO KIKOMBO DODOMA
-
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.
Mwanaidi Ali Khamis akigawa iftar kwa mmoja ya mtoto anayelelewa katka
Makao ...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.