KILE KISIKI CHA ULE MTI WENYE HISTORIA ULIOKUWA UKITUMIKA ENZI ZA UKOLONI KUNYONGEA WATU WALIOKUWA WAKIENDA KINYUME NA KANUNI NA SHERIA ZA UTAWALA WA ENZI HIZO, KISIKI HICHO KIKO KWENYE UKARABATI, KIKIPAKWA RANGI KUWA NA MUONEKANO WA KISANAA ZAIDI ILIKIPATE KUFANYWA SEHEMU YA KUMBUKUMBU YA HISTORIA HIYO NA KIVUTIO KWA UTALII.
FUNDI AKITIA NAKSHI KATIKA KISIKI HICHO.
ENZI HIZO ENEO LA MTI HUU LILIKUWA LA KUOGOFYA SANA NA LILIKUWA LIKIHESHIMIWA NA WATU WOTE.
KISIKI CHA MTI HUU AINA YA MNIRA KINACHO PATIKANA KATIKATI YA JIJI LA MWANZA KATIKA KIPITA SHOTO CHA KARIBU NA ENEO LA BENKI KUU NA JENGO LA MAKAO MAKUU YA CCM MJINI HAPA, SIFA ZAKE MTI HUU ENZI ZA UHAI WAKE ULIKUWA MPANA NA WENYE MATAWI YALIYO IMARA, YASIYO RAHISI KUKATIKA YENYE UWEZO WA KUNING'INIZA KITU CHOCHOTE CHA UZITO WOWOTE. KUTOKANA NA USHIRIKI WAKE KATIKA KUMWAGA DAMU ZA NDUGU ZETU NA KUTOA ROHO ZA WATU WENGI, ENEO HILI LINASADIKIKA KUWA NA MAMBO YA KIMAZINGIRA.
RAIS SAMIA AFTURISHA WATOTO KIKOMBO DODOMA
-
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.
Mwanaidi Ali Khamis akigawa iftar kwa mmoja ya mtoto anayelelewa katka
Makao ...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.