ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 2, 2010

MV NG'OMBE NI MALI, YATEKETEA WAKATI IKING'OA NANGA.

Moto umetokea jana majira ya saa 2 usiku na kudumu kwa zaidi ya masaa matatu umeiteketeza kabisa boti ya Mv Ng'ombe ni mali.

Boti hiyo inayofanya kazi zake za kusafirisha bidhaa mbalimbali kutoka na kuingia ktk visiwa vilivyopo ndani ya ziwa Victoria, ilikumbwa na dhahma hiyo wakati iking'oa nanga, chanzo kikitajwa kuwa ni shoti iliyotokea upande wa plug ktk injini ya boti hiyo, ile kuwasha tu! ikawa kama kibiriti kwa mapipa ya mafuta ya taa na petrol yaliyokuwemo kwenye chombo hicho

"Katoni 10 za tingisha, dumu 6 za maji ya breweries na box 20 za maji ya kilimanjaro" Mfanyabiashara Januar Mgalula akisimulia mali zake zilizoteketea. Zaidi ya mapipa 240 pamoja na bidhaa mbalimbali zilizokuwa zikisafirishwa kuelekea visiwa vya Bulubi na kisiwa cha Ghana zimeteketea ktk moto huo.

Wananchi wakishuhudia moto chini ya ulinzi wa kutowaruhusu kulikaribia eneo la tukio.

Kamanda wa polisi wilaya ya Ilemela mama Matola akichukua taarifa.

Boti ikiteketea.

Zimamoto katika tukio hili kama vile walikuwa darasani wakifanya majaribio.

Alhamdulilah! Vijana hawa waliokuwa wakisaka masalia asubuhi ya leo wameibuka na mfuko wa sukari uliokuwa chini kabisa.

WAMILIKI WA MALI ZILIZOKUWEMO KATIKA CHOMBO HICHO KILICHOTEKETEA.

HALI ASUBUHI YA LEO.
Mazingira haya tusinge yaona leo hivi kwani kuna baadhi ya boti zilizokuwa karibu na boti iliyoungua, zikisubiri safari siku inayofuata wamiliki wamiliki wake hawakuwepo eneo la tukio, msaada wa kukata kamba za nanga ulifanyika kuzinusuru. Kwani Kulikuwa na kila dalili ya moto huo kusambaa eneo zima na kuteketeza kila kilichopo pande hizo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.