Ni Januari 12, 2026… Mwanza inawaka moto wa sherehe!!
Katika kuadhimisha Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, jiji la Mwanza linawaletea burudani ya kipekee, mechi ya kirafiki ya kihistoria… Mashabiki wa Simba vs Pamba Jiji!
Watachuana mastaa wa zamani waliowahi kung’ara kwenye timu hizi mbili maarufu nchini – ni kumbukumbu, ni burudani, ni hadithi za mpira zinazofufuka tena!
Na si mpira tu! Kutakuwa na michezo ya kina dada, kina mama, zawadi kibao na burudani ya nguvu kwa familia nzima!
Jumatatu ya tarehe 12 Januari 2026, kuanzia saa nane mchana, pale Uwanja wa Nyamagana – usikose kushuhudia historia ikiandikwa upya!
MAPINDUZI DAY – Mwanza inasherehekea kwa mshikamano, amani na burudani ya kufungia mwaka!
Mgeni rasmi: Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Said Mtanda
Tupe maoni yako

0 comments:
Post a Comment