NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibaha mjini kupitia tiketi ya Chama cha mapinduzi Silvestry Koka amesema kwamba endapo akipata ridhaa ya kuchaguliwa ataboresha sekta ya elimu na afya kwa wakazi wa kata ya Visiga.
Koka ameyasema hayo wakati wa mkutano wa kampeni katika kata ya Visiga uliohudhuliwa na viongozi mbali mbali wa chama pamoja na wananchi.
Koka amesema kwamba endapo akichaguliwa kupata nafasi hiyo atahakikisha anaboresha elimu kwa kutoa madawati elfu 1000 kwa shule za msingi ili lengo ikiwa ni kuongeza kiwango cha ufaulu.
Amebainisha kwamba pia atashirikiana bega kwa bega na serikali katika kujenga shule moja mpya ya msingi ikiwa sambamba na shule moija mpya ya sekondari katika kata ya Visiga.
Kadhalika Koka amebainisha kuwa katika kuwawekea mazingira mazuri wanafunzi atahakikisha anaboresha miundombinu ya matundu ya vyoo katika baadhi ya shule.
Akizungumzia kuhusiana na miundombinu ya nishati ya umeme amebainisha atalivalia njuga suala la nishati ya umeme katika baadhi ya mitaa ikiwemo eneo la Zegereni,Saheni na maeneo mengine ya pembezoni.
Kwa upande wake Mgombea Udiwani kata ya Visiga Mohamed Mpaki amesema kwamba atahakikisha anatekeleza ilani ya chama kwa vitendo katika miradi mbali mbali ya maendeleo.
Naye Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Mwalimu Mwajuma Nyamka lengo kubwa ni kuweza kushinda kwa kishindo katika nafasi ya Urais,Ubunge na Udiwani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment