Hivi ndivyo Rais Samia Suluhu Hassan alivyo wasili katika viwanja vya Nane Nane - Nzuguni Dodoma, kwa ajili ya kushiriki kilele cha maadhimisho ya maonesho ya kilimo, mifugo na uvuvi kitaifa na kimataifa.
Maonesho hayo ni jukwaa muhimu la kuonesha teknolojia, ubunifu na fursa mbalimbali katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi, yakilenga kuongeza tija na ustawi wa wakulima, wafugaji na wavuvi nchini.
Rais Samia Suluhu Hassan leo tarehe 08, Agosti 2025 kwenye kilele cha Maonesho ya Kitaifa na Kimataifa ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma pamoja na mambo mengine pia ametembelea baadhi ya Mabanda na kujionea shughuli mbalimbali zinazoendelea viwanjani hapo.
Akizungumza Jijini Dodoma, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema kwa mara ya kwanza Maonesho ya Nanenane mwaka huu yamewakutanisha Watu kutoka Mataifa 26 Duniani na kuongeza kuwa maonesho hayo katika Nchi nzima yatakuwa na ubora uleule.
Akizungumza Jijini Dodoma, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema kwa mara ya kwanza Maonesho ya Nanenane mwaka huu yamewakutanisha Watu kutoka Mataifa 26 Duniani na kuongeza kuwa maonesho hayo katika Nchi nzima yatakuwa na ubora uleule.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitembelea mabanda ya Maonesho ya Nanenane kujionea shughuli mbalimbali zinazoendelea katika viwanja vya Nanenane vilivyopo Nzuguni Jijini Dodoma tarehe 08 Agosti, 2025.Matukio mbalimbali kwenye Maonesho ya Kitaifa na Kimataifa ya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma tarehe 08 Agosti, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo baada ya kuzindua Maabara Kuu ya Kisasa ya Kilimo iliyopo Mtumba, Jijini Dodoma, tarehe 08 Agosti, 2025.
Tupe maoni yako
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
0 comments:
Post a Comment