ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 31, 2025

BASI LILILOBEBA MASHABIKI WA TAIFA STARS LATEKETEA KWA MOTO

Katika tukio la kushtua na kusikitisha, basi dogo aina ya Eicher lenye namba za usajili T 284 EFJ, mali ya Chama cha Walimu Wilaya ya Misungwi, limeteketea kwa moto likiwa safarini kutoka jijini Mwanza kuelekea Dar es Salaam. Basi hilo lililokuwa limebeba mashabiki wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), limekumbwa na ajali hiyo katika eneo la Mabuki mkoani Mwanza. Kwa mujibu wa shuhuda ambaye pia ni mmoja wa abiria, aitwaye Hemedi Kiongozi amesema moto ulianzia kwenye eneo la injini mbele kwa dereva. Licha ya juhudi za haraka kutumia vizima moto kama fire extinguisher na mchanga, moto huo ulizidi nguvu na kusababisha basi hilo kuteketea kabisa. Taarifa zaidi ikiwa ni kumtafuta Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza zinafanyika kupata taarifa kwa kina zaidi kuhusu hali ya abiria na chanzo rasmi cha moto huo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment