NA ALBERT GSENGO/MWANZA
Katika hatua inayoashiria kasi ya ukuaji wa sekta ya ujenzi na biashara jijini Mwanza, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala, ametoa wito kwa wawekezaji hususan wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi kujitokeza na kuwekeza jijini hapa ili kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu kwa wananchi. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka jipya la vifaa vya ujenzi la ABC Mwanza Hardware, Masala amesema uwepo wa maduka hayo utapunguza utegemezi wa bidhaa kutoka Dar es Salaam umbali wa wa zaidi ya kilimita 1,200 na kupunguza gharama za usafirishaji kwa wananchi wa Mwanza na mikoa jirani. “Tunahitaji makampuni kama haya kuja zaidi Mwanza. Wananchi wetu wanastahili huduma bora, za haraka na zenye bei nafuu. Uwekezaji huu ni dalili ya uhai wa kiuchumi wa jiji letu,” alisema Masala. Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Constantine Sima, amesisitiza kuwa ujio wa ABC Mwanza Hardware unamaanisha fursa zaidi kwa Kanda ya Ziwa, huku akilitaja jiji la Mwanza kama kitovu cha biashara kwa mikoa ya kaskazini magharibi. Mwakilishi wa kampuni ya ABC Mwanza Hardware, Bwana Sahares amesema wamejipanga kutoa huduma za kiwango cha juu kwa kutumia teknolojia ya kisasa na kutoa vifaa vya ujenzi kwa bei rafiki, wakilenga kuwahudumia wateja wote wa Kanda ya Ziwa kikamilifu. Mbali na uzinduzi huo, tuangazie pia ni kwa namna gani ujio wa duka hilo jipya la vifaa vya ujenzi utaleta tija kwa wananchi na wafanyabiashara wa jiji la Mwanza. Zulfikar Nanji ni Mkurugenzi wa Kampumi ya Mwanza Huduma, anafafanua kwa kina mafanikio yanayotarajiwa kupitia uwekezaji huu. #samiasuluhuhassan #mwanzaTupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment