Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza Ndg Michael Masanja Lushinge Smart (MNEC) (katikati aliyesimama) Mapema Leo Tarehe 03, juni 2025 Ameongoza kikao Cha Kamati ya maandalizi ya Mazishi ya Mzee Silvin Ibengwe Mongella Ambaye ni Baba Mzazi wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Ndg John Mongella Ambacho kimefanyika nyumbani Kwa marehemu Kijiji cha Kabusungu Kata Sangabuye Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza
Aidha Mwili wa marehemu unatarajiwa kuwasili Uwanja wa ndege Mwanza siku ya Alhamis 05 juni, 2025 majira ya saa 12 Asubuhi na kuhifadhiwa
Ijumaa 06, juni Mwili wa marehemu utawasili kijiji cha Kabusungu Kata Sangabuye Wilayani Ilemela Kwa Ibaada ya maombolezo kisha Ibaada ya mazishi itafanyika Tarehe 07, juni 2025 katika Kijiji cha Kabusungu
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake libarikiwe
Imetolewa na Ofisi ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza
Tupe maoni yako
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
0 comments:
Post a Comment