VICTOR MASANGU/KIBAHA/PWANI
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, vijana,ajira na watu wenye ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka vijana wa halaiki ambao wamechaguliwa kushiriki katika maandalizi ya uwashwaji wa Mwenge wa uhuru Kitaifa kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika kuwa wazalendo na nchi yao na kutunza na kuzilinda rasilimali za Taifa.
Ridhiwani ameyasema hayo wakati alipofanya ziara kwa ajili ya kutembelea na kugagua mwenendo na maandalizi katika eneo la uwanja wa shirika la elimu Kibaha ambapo utakaotimika kwa ajili ya uwashwaji wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa ikiwa sambamba na kuzungumza na vijana hao na kuwahimiza kuwa wavumilivu katika kipindi chote cha maandalizi.
Naye Injinia kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Charles Kabeho ambaye pia ni msimamizi wa ukarabati wa eneo la uwanja utakaotumika kuwashiwa Mwenge wa uhuru amebainisha kwamba kwa sasa ukarabati kwa sasa umeshafikia asilimia 75.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge amebainisha kwamba maandalizi yote kwa ajili ya kuelekea katika tukio la kuwasha Mwenge wa Uhuru Kitaifa yanaendelea vizuri katika maeneo ya miundombinu ya barabara, nishati ya umeme, maji na kwamba hadi sasa hali ya ulinzi na usalama imeimarishwa kwa kiwango kikubwa.
Sherehe za uwashwaji rasmi wa Mwenge wa uhuru kitaifa zinatarajiwa kufanyika rasmi Aprili 2 mwaka huu katika viwanja vya shirika la Elimu Kibaha vilivyopo Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani ambapo viongozi mbali mbali wa ndani na nje ya nchi wanatarajia kushiriki katika tukio hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.