Mohammed Iqbal Dar, aliyebuni jina la Tanzania, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80 jijini Birmingham, Uingereza, ambako aliishi tangu mwaka 1965.
Dar amefariki baada ya kuugua kwa takriban miaka 10, kipindi ambacho alikuwa hawezi kutembea na alikuwa chini ya uangalizi wa karibu nyumbani kwake.
Alizaliwa Agosti 8, 1944, mkoani Tanga. Baba yake, Dk. Tufail Ahmad Dar, alikuwa daktari mashuhuri aliyewahi kufanya kazi katika mikoa ya Tanga na Morogoro.
Mohammed Iqbal Dar alipata elimu yake ya msingi na sekondari katika Shule ya Aga Khan, kabla ya kuendelea na masomo yake katika Shule ya Sekondari Mzumbe mwaka 1964.
Akiwa mwanafunzi Mzumbe, aliona tangazo katika gazeti la The Standard likiwahamasisha wananchi kupendekeza jina jipya la taifa lililoundwa baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
![]() |
Kuna nyakati kulizuka mzozo juu ya nani ndiye alikuwa mbunifu wa jina Tanzania. |
Kwa bahati ya kipekee, pendekezo lake la jina Tanzania lilichaguliwa kuwa jina rasmi la nchi, na alitunukiwa tuzo ya Shilingi 200 pamoja na medali iliyotolewa na aliyekuwa Waziri wa Habari wakati huo, Sheikh Idrisa Abdul Wakil.
Kifo cha Mohammed Iqbal Dar ni pigo kwa historia ya taifa, kwani mchango wake uliasisi utambulisho wa nchi inayojivunia jina la Tanzania hadi leo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.