HABARI NA VICTOR MASANGU/ PWANI
SAUTI NA ALBERT G.SENGO Tume huru ya Taifa ya uchaguzi imekemea vikali na kupiga marufuku kwa mtu yoyote kujiandikisha zaidi ya mara moja katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai na endapo wakibainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Kauli hiyo imetolewa na Makamu mwenyekiti wa Tume huru ya Taifa ya uchaguzi Mhe. Jaji Mbarouk Mbarouk ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa mkutano wa Tume na wadau mbali mbali wa uchaguzi wa Mkoa wa Pwani kuhusiana na suala zima la mwenendo mzima wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa mwaka 2025.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.