ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 28, 2025

WAZIRI WA AFYA ATUA HOSPITALI YA MLOGANZILA AWAPONGEZA WATUMISHI KUBORESHA AFYA

 


NA VICTOR MASANGU

Waziri wa Afya Mh. Jenista Mhagama amefanya ziara ya siku moja Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila kwa lengo la kukagua hali ya utoaji wa huduma katika hospitali hiyo.

Mh. Mhagama ameupongeza uongozi wa hospitali hiyo na kuwataka wataalam kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kwakuwa kufanya hivyo ni kuunga mkono juhudi za kuboresha huduma za afya zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Aidha, Mh. Mhagama amewajulia hali na kuwapa pole wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo kutokana na changamoto mbalimbali za kiafya na kuwaombea wapone haraka na kurejea katika majukumu yao ya siku hadi siku.

Katika ziara hiyo Mh. Mhagama ametembelea baadhi ya maeneo ya kutolea huduma ikiwemo Idara ya Radiolojia, Magonjwa ya Dharura na Ajali, wodi namba nane inayotumika kuhudumia majeruhi wa ajali mbalimbali pamoja na wodi za wagonjwa mashuhuri.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.