NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Waandaaji wa Mbio za Coast City Marathon Mkoa wa Pwani ambazo huwa zinafanyika kila mwaka Mkoani humo, msimu huu wamekuja kivingine baada ya kugeukia maboresho ya miundombinu ya elimu.
Mbio hizo ambazo zinatarajia kufanyika Novemba 30,2024 Kibaha Mkoani humo zinalenga kukusanya sh. 80 milioni na kwamba pesa hizo zitaelekezwa kuboresha miundombinu ya shule ya Msingi Pangani
Tofauti na misimu miwili iliyopita maboresho mengine katika mbio hizo ni motisha kwa washiriki wote kwani mbali na kupata medali na zawadi mbalimbali pia watanufaika na supu ya pweza,madafu na nyama choma siku ya tukio hilo
Akizungumza leo mjini Kibaha wakati wa uzinduzi wa dirisha la usajili pamoja na vifaa vitakavyotumika siku ya tukio mwenyekiti wa maandalizi hayo Frank Muhamba amesema kuwa kutokana na umuhimu wa elimu kwa jamii wameona ni vema waelekeze nguvu huko ili kusaidia juhudi za serikali
Amesema kuwa kufanya hivyo si kuwa uongozi wa shule hiyo uliwaomba bali ni kutokana na uzalendo walionao na wanaamini kuwa kusudio lao litatimia
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo Afisa elimu msingi Halmashauri ya mji wa Kibaha Theresia Kyara amesema kuwa ni jambo la kuwapongeza waandaajli hao kwani wanaenda kusaidia kupunguza changamoto zilizopo ndani ya sekta muhimu
Balozi wa mbio hizo Twaha Ambiere amesema kuwa tofauti na awamu zilizopita kwa mwaka huu wameboresha mambo mbalimbali ikiwemo zawadi na motisha kwa washirili wote
Afisa michezo halmashauri ya Mji wa Kibaha Burwan Tilusubya amewataka wakazi wa Mkoa wa Pwani kujitokeza kwa wingi ili kujisajili na kushiriki kikamilifu kwenye mbio hizo kwani zinafaida nyingi ikiwemo kujenga afya.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.