VICTOR MASANGU,PWANI TV
Kilio cha walimu wa shule ya msingi Boko Timiza iliyopo kata ya Tumbi Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mji kilichokuwa kikiwakabiliwa kwa kipindi cha miaka zaidi ya 40 cha kuwepo na changamoto sugu ya ukosefu mkubwa wa kutokuwa na viti na meza hatimaye kimepatiwa ufumbuzi baada ya baadhi ya wadau wa maendeleo ya elimu kuamua kulivalia njuga suala hilo na kwenda kutoa msaada kutokana na kubaini walimu hao hawana sehemu maalumu ya kukaa.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Boko Timiza Rozania Kimate wakati wa halfa fupi iliyofanyika shuleni hapo kwa ajili ya kukabidhiwa msaada huo wa viti na meza kutoka kwa mdau wa maendeleo Selina Koka ambaye pia ni mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini na Mlezi wa Jumuiya ya Umoja wa wanawake (UWT) Wilaya ya Kibaha mjini na kubainisha msaada huo utakuwa ni mkombozi mkubwa kwa walimu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.