ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 23, 2024

VIJANA WAKUMBUSHWA KUJIKITA KATIKA MIDAHALO KUONGEZA UELEWA WA MAISHA.

 


NA VICTOR MASANGU

Vijana wametakiwa kushiriki  katika midahalo mbalimbali itakayowawezesha kuwa na mawazo chanya juu ya mustakabali wa maisha yao.

Hayo yamesemwa na Mwanzilishi wa jukwaa la Power of Sentence ambalo ni jukwaa la uwezeshaji kwa vijana kupitia simulizi za maneno ambapo, jukwaa hilo linatoa nafasi kwa vijana kupata nafasi ya kutambua athari za maneno zinavyoweza kuathiri maamuzi yako na zingine zinazoweza kuwajenga kifikra.

Mwanzilishi wa jukwaa la Power Of Sentence, Jackline Christopher amesema jukwaa hili limewakutanisha vijana mbalimbali na kufanya midahalo juu ya maneno yanavyoweza kuathiri maamuzi yao.

Jackline amesema, huu ni mwaka wa tano toka kuanzishwa kwa jukwaa hilo na limewawezesha vijana wengi kufikia malengo yao baada ya kuweka wazi hisia na fikra zilizopo ndani ya mawazo baada ya kuyawasilisha mbele ya jamii.

“Hii powe of sentence ni namna ambayo mtu anaweza kutumia maneno yake kuweza kumletea mafanikio na muda mwingine yanaweza yakaathiri maisha yake kwa namna moja ama nyingine,” amesema Jackline.

“Unaweza kuwa na mawazo yakawa ni mazuri au mabaya kulingana na utakavyochukulia, zaidi unapokuwa na mawazo usiyaache kuyatumia na kuyaishi kwa sababu maneno hayo yanayopita ndani ya kichwa chako yanaweza kukujenga zaidi na kufikia malengo yako,” amesema


Akizungumzia msimu wa tano wa jukwaa hilo linalotarajia kufanyika Julai 27, mwaka huu Jackline amewaomba vijana wajitokeze kwa wingi kwa kununua tiketi kwani dhamira ya jukwaa hilo ni kuona linafika mbali zaidi katika mikoa mingine ikiwemo Kigoma.

Jackline ni mwandishi wa vitabu mbalimbali ambapo tayari ameshazindua kitabu chake cha 100 Power of Sentence na Amnesia ambavyo vyote kwa sasa vinapatikana.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.