ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 22, 2024

NHC YATUMIA ZAIDI YA MILIONI 300 KUBORESHA MAJENGO YAO TANGA

 


Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mkoani Tanga Mhandisi Mussa Kamendu

Na Oscar Assenga, TANGA

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita 2023/2024 wametumia zaidi ya Milioni 300 kwa ajili ya matengenezo makubwa ya majengo yao katika Jiji la Tanga.

Hayo yalibainishwa leo na Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mkoani Tanga Mhandisi Mussa Kamendu wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kwamba matengenezo hayo yatahusisha nyumba za Ngamiani, Nguvumali, Bombo mpaka Raskazone.

Mhandisi Kamendu alisema kwamba shirika hilo limefanya mkakati huo maalumu makusudi kuhakikisha majengo yao yanaboreshwa na kuwa na muonekano mzuri ikiwemo kupakwa rangi ili wapangaji wao waishi kwenye mazingira mazuri.

“Katika miji yote ya Tanzania Shirika hilo linamiliki nyumba katikati ya Miji na Majiji kwa hiyo nyumba zinapokuwa kwenye hali mbaya zinafanya miji ionekane vibaya na taswira ya majiji inakuwa haipo vizuri kwa kuliona hilo shirika limekuja na mkakati maalumu wa kuzipaka rangi ili ziweze kuwa na muonekano mzuri na kubadilisha mifumo ya maji taka na maji safi “Alisema

Aidha allisema pia katika matengenezo hayo wamebadilisha pia mifumo ya umeme ambayo imechakaa na kurekebisha miundombinu mbalimbali mingine ikiwemo milango na madirisha ili kuhakikisha wanapangaji wanakuwa kwenye mazingira mazuri.

Katika hatua nyengine Meneja huyo aliwataka wapangaji wao kuhakikisha wanabadilika na kufuata mikataba yao inavyowataka walipe kodi kwa wakati ili waweze kuepukana na usumbufu wanataokumbana nao.

Mhandisi Kamendu alisema kwamba mikataba yao inawataka wapangaji wao kuhakikisha wanalipa kodi kwa wakati na pia waweze kuepukana usumbufu watakaoupata maana pale ambao hawajalipa kodi kufuatia na mikataba yao itafikia wakati watatolewa kwenye nyumba hizo.

“Wapangaji wasumbufu ambao wanasubiri mpaka kufuatwa na madadali kwenye kwenye nyumba sasa wanapotelewa kwenye nyumba ni usumbufu na aibu kwa familia na jamii inaweza kuona ni mtu wa ajabu tusisburi mpaka kufukia hatua hii”Alisema

Katika hatua nyengine Meneja huyo alisema kwamba shirika hilo limejiwekea malengo la kukusanya Sh. Bilioni 2,444,183,556.96 katika Bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 kutokana na makusanyo yao ya Pango la Kodi kutoka katika nyumba zao.

Alisema kwamba hayo ndio malengo yao na mwaka huu wa fedha kwa sababu hiyo kama mkoa wanaendelela kuboresha huduma zao.

Alisema kwamba wanafanya hivyo kama shirika ili kuhakikisha wapangaji wanakuwa kwenye mazingira mazuri na kuwa sawa ili kodi zao wanazolipa ziendane na thamani ya mahali wanapoishi.

Maneja huyo alisema kwamba malengo yao ya Bajeti katika Mwaka wa Fedha wa 2023/2024 waliweza kukusanya kiasi cha Bilioni 2,040,727,435 kutokana na kodi ya pango kutoka kwa wapangaji wao walioishi kwenye nyumba za shirika hilo.

Alisema katika mwaka wa fedha kuanzia Julai 2023 mpaka June 2024 waliweza kukusanya kiasi cha Bilioni 2,040,727,435 na malengo waliokuwa wamejiwekea kwenye bajeti yao ya mwaka 2023/2024 ilikuwa ni kukusanya kodi Bilioni 2,046 ,528,000 .

“Kwa hiyo utaona ukiangalia kiasi tulichokusanya wao Biloni 2,040,727,435 tumekusanya kwa asilimia 99.7 ya malengo ya bajeti yetu ya mwaka 2023/2024 kwa hiyo katika majengo yetu na idadi ya wapangaji wao na kodi tunavyokusanya kwa ufupi tumefikia malengo ya kwa sababu asilimia 99.7 ni sawa asilimia 100 kiasi cha 5,856,400 ndio ambacho hakijaweza kukusanywa”Alisema

Aidha alisema na hivyo inatokana na madeni ya wapangaji wao ambao wanadaiwa na ni wajibu wao kuendelea kuyadai na kuchukua nafasi hiyo kuwapongeza wapangaji ambao wanalipa vizuri huku wakiendelea kuwasisitizia kuendelea kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.