NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Manispaa ya Iringa Mkoa wa Iringa licha ya kushika nafasi ya tatu kitaifa katika mashindano ya kampeni ya mtu ni afya awamu ya pili imeahidi kuyatekeleza maagizo ambayo yametolewa na Makamu wa Rais Dkt. Philipo Mpango kwa lengo la kuweza kuhakikisha inazingatia usafi wa mazingira ili kuweza kupambana na mlipuko wa magonjwa.
Hayo yamebainishwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahimu Ngwada wakati akizungumza na waandishi wa bahari mara baada ya kupokea cheti na kiasi cha shilingi milioni moja baada ya kushinda katika nafasi ya tatu kwa katika manispaa ambazo ziliweza kufanya vizuri katika suala zima la usafi wa mazingira.
Meya huyo alieleza kwamba siri kubwa ya kuweza kushika nafasi ya tatu katika nchi nzima na kwa ajili ya kuwa na utamaduni wa wananchi wa Iringa waliojiwekea katika kuweka utaratibu wa kufanya zoezi la usafi katika maeneo mbali mbali ambayo yameweza kupelekea kila mwaka kufanya vizuri katika mashindano hayo.
"Utamaduni wetu kwa watu wa manispaa ya Iringa pamoja na Mkoa mzima ni kuhakikisha kila
msimu wa mashindano hayo ya kampeni hii ya usafi tunafanya vizuri na kuwa washindi kwa hii kwa upande wangu ninawaahidi katika msimu ujao pia tutaweza kufanya vizuri kwani tutazingatia yale yote ambayo yametolewa na Makamu wa Rais,"alisema Meya huyo.
Pia alishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kushirikiana na Wizara ya afya kwa kuanzisha kampeni hiyo ambayo imeweza kusaidia kwa kiaisi kikubwa katika kupambana na usafi wa mazingira ambao unasaidia hata kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.
Sambamba na hilo alibainisha kwamba mpaka kufikia hatua hiyo ya kushinda nafasi ya tatu kwa ngazi ya Taifa ni kutokana na kuweka mipango madhubuti katika maeneo mbali mbali ikiwemo kuweka sehemu maalumu kwa ajili ya kutupia taka katika kila mtaa pamoja na sehemu za kunawia mikono katika maeneo mbali mbali ya mikusanyiko kama vile mashuleni, hospitalini pamoja na kwingine ikiwa sambamba na kuzingatia taratibu na maelekezo yote yanayotolewa na wataalamu wa afya.
Katika hatua nyingine Meya huyo alitoa wito kwa wananchi wote wa Manispaa ya Iringa lengo ikiwa ni kupunguza magonjwa ya matumbo ambayo kwa sasa amesema yameshuka kwa kiwango kikubwa na kuwahimiza kuendelea kufanya usafi katika maeneo ambayo wanaishi na sehemu nyingine za biashara.
Naye Mganga Mkuu wa Manispaa ya Iringa Dkt. Godfrey Mbangali aliongeza kuwa kwa sasa kutokana na kujipanga wamefaanikiwa kwa kisi kikubwa kupunguza magonjwa ya kuharisha ndio maana wameweza kupata ushindi huo wa nafasi ya tatu kwa nchi nzima.
"Mimia kama Mganga mkuu wa Manispaa ya Iringa tumejitahidi sana kwa hali na mali mimi pamoja na timu yangu kwa kuhakikisha kwamba tunapambana na magonjwa mbali mbali ya mlipuko ikiwemo matumbo pamoja na kuharisha na kiukweli mashidano hayo yanafanyika kisayansi zaidi na ndio maana sisi tumeshika nafasi hii ya tatu kwa kuzingatia vigezo ambavyo vinatakiwa na kwa sasa ukiangalia magonjwa ya mlipuko yamepungua sana,"alisema Mganga huyo.
Kwa upande wake Makamu wa Rais , Dkt Philipo Mpango ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alizitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha wanaweka mifumo mizuri katika maeneo yao ambayo itaweza kusaidia katika suala zima la kuboresha usafi wa mazingira na kupambana na magonjwa ya mlipuko.
Kadhalika Waziri Mpango alipongeza makundi, taasisi, halmashauri, manispaa, pamoja na mikoa mbali mbali ambayo imeweza kufanya vizuri katika mashindano hayo na kuwataka kuendelea kushirikiana na ngazi zote pamoja na wananchi lengo ikiwa ni kutomomeza kabisa magonjwa ya mlipuko amabayo wakati mwingine yanatokana na baadhi ya maeneo kuwa machafu.
Kwa upande wake Waziri wa afya Mhe. Ummy Mwalimu alisema kwamba serikali ilishaanza kuchukua hatua mbali mbali kwa ajili ya kudhibiti na kuboresha huduma za afya nchini na kufanikiwa kupunguza na kutokomeza baadhi ya magonjwa yasiyoambukiza.
Alisema alieleza kwamba kupitia kampeni hiyo ya mtu ni afya awamu ya pili benki ya dunia imetoa isi cha shilingi bilioni 5.5 kwa ajili ya utekelezaji huo ambao utafanyika kwa awamu kwa kipindi cha miaka saba.
Waziri Ummy katika hatua nyingine hakusita kuupongeza kwa dhati Mkoa wa Iringa ambao umeweza kuibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya usafi wa mazingira na matumizi mazuri ya vyoo bora na kuweza kukabilina na magonjwa ya mlipuko na kuongeza kuwa Mkoa huo ndio umeshika nafasi ya kwanza kwa nchi nzima na kukabidhiwa zawadi mbali mbali ikiwemo gari mpya aina ya Land crucer.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.