NA VICTOR MASANGU/KIBAHA
Katibu wa Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Bernard Elias Ghati amewahimiza wana ccm pamoja na wananchi kwa pamoja kumchagua kwa kishindo mgombea wa udiwani kata ya Msangani Gunze Yohana ili aweze kuwaletea wananchi maendeleo.
Katibu huyo ameyasema hayo wakati wa mkutano wa kampeni wa hadhara kwa ajili ya kuweza kumnadi mgombea wa udiwani uliofanyika katika mtaa Garagaza.
Katika mkutano huo wa kampeni ambao ulihudhuliwa na viongozi mbali mbali wa ngazi ya Wilaya pamoja na ngazi ya Mkoa sambamba na wananchi wengine kutoka Jimbo la Kibaha mjini.
Katibu huyo aliwaomba katika kuelekea katika uchaguzi huo wananchama wa ccm wanapaswa kuwa kitu kimoja katika kuhakikisha kwamba wanashinda kwa kishindo kwa asilimia kubwa katika uchaguzi huo.
"Kikubwa tunakuja katika mikutano hii kwa ajili ya kuzungumza mambo mbali mbali ambayo chama cha mapinduzi mambo ambayo yamefanyika katika utekelezaji wa Ilani hivyo wananchi wa Msangani inabidi kumchagua mgombea wetu Gunze '"alisema katika huyo.
Aidha katibu huyo alisema kuwa wana ccm wanatakiwa kuungana kwa pamoja na wananchi wote wa kata ya Msangani kwa lengo la kuwaeleza mambo mbali mbali yaliyofanyika ya kimaendeleo.
"Inatakiwa wana msangani wote muelewe shughuli mbali mbali za kimaendeleo ambazo zimefanywa na hivyo ninawaomba wananchi kumchagua Gunze awe diwani wa kata ya Msangani,"alisema Katibu huyo.
Katika hatua nyingine aliongeza kuwa endapo wananchi wa kata ya Msangani wakimchagua Gunze kuwa diwani wa Kata ya Msangani ataweza kuwaletea maendeleo wananchi katika nyanja mbali mbali ikiwemo maji,afya,elimu pamoja na maeneo mengine.
Uchaguzi wa kujaza nafasi ya udiwani katika kata ya Msangani amnayo ilikuwa wazi unatarajiwa kufanyika machi 20 mwaka huu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.