ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, January 29, 2024

TAASISI YA LIONS CLUB YAKABIDHI MATANKI NANE YA MAJI KWA AJILI YA KUWASAIDIA WANAFUNZI WA VIGWAZA

 

NA VICTOR MASANGU,VIGWAZA


TAASISI ya Lions Club inayojishughulisha na masuala mbali mbali  ya kijamii imekabidhi matenki nane kwa ajili ya kuhifadhia maji katika shule zilizopo kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Matanki hayo yanakwenda kusaidia kutunza maji safi na salama kwa ajili ya wanafunzi wakiwa shuleni na kuondokana na adha ya watoto kubeba maji pindi yanapokuwa yamekatika.

Akisoma taarifa ya makabidhianao ya matanki pamoja na vyakula kwa ajili ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu Muntazir Bharwani alisema wametoa msaada huo baada ya kupokea maombi kutoka kwa Diwani wa Vigwaza Mussa Gama.

Bharwani ambaye alisoma taarifa hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Lions Host Kaniz Naghavi alisema hafla hiyo ya makabidhiano iliambatana na kumkaribisha Gavana wa Tanzania District 411C Happiness Nkya katika shughuli ya chama .

Aliwaomba wakazi wa Vigwaza kuhifadhi na kuyatumia vizuri matanki hayo Ili yaweze kuwasaidia wanafunzi na kuwaondoa katika tatizo la kukosa maji wakiwa shule.

"Lions Clubs imepata ufadhili huu kutoka kwenye kampuni ya Refuelling Solutions (T) Limited na wadau wengine na wanachama wa taasisi hii wamechangia kuleta vyakula kwa watoto yatima Vigwaza," alieleza.

Taasisi hiyo imetoa hamasa kwa taasisi nyingine kutoa huduma na misaada kwa wanafunzi  wa Shule za hapa nchini kutokana na uhitaji wa vitu vingi utaratibu ambao utasaidia kuboresha masuala ya elimu, afya na michezo.

Gavana wa Taasisi hiyo  Hapiness Nkya alisema kwasasa wapo wanachama 620 na club 23 huku 14 zikiwa Dar es Salam wamekuwa wakitoa misaada kwenye maeneo mbalimbali ambayo wanashiriki moja kwa moja na mingine kuomba kwenye makampuni.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze Ramadhani Poss, Afisa Elimu awali na Msingi wa Halmashauri hiyo aliishukuru taasisi hiyo kwa misaada ambayo inaitoa kupunguza vikwazo kwa wakazi wa Vigwaza.

Diwani wa Vigwaza Mussa Gama ameishukuru Taasisi hiyo huku akieleza kwamba umekuwa ikisaidia mambo mbalimbali ya maendeleo katika Kata hiyo kwa kutoa vifaa kwenye Zahanati, daftari kwa wanafunzi na sasa matenki na vyakula kwa yatima.

" Hawa Lions wamekuwa ni watu wa karibu wanaomsaidia kutafuta matatizo kwenye kata yetu naomba wadau wengine wajitokeza kutupatia misaada ya fedha na vitu kwenye sekta za afya na elimu," alisema Gama.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ruvu Darajani Samwel Mjema alisema matanki hayo yanakwenda kuwasaidia kutunza maji pindi yanapokatika huku akiahidi kuyatunza Ili yadumu kwa muda mrefu na kuwa msaada kwa wanafunzi.

Shule nane zilizonufaika na matanki hayo ni pamoja na Msilale, Chamakweza,Sekibwa, Ruvu, Kitonga na Kwazoka zote za Msingi na Sekondari ni Mnindi na Ruvu na hivi karibuni matanki mengine mawili yataletwa na kukabidhi a shule husika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.