ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, January 21, 2024

MAAGIZO YA WAZIRI WA MAJI ALIPOKUWA MKATA YAANZA KUTEKELEZWA NA DAWASA

 


VICTOR MASANGU,MKATA


Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) Kiula kingu amefika katika kata ya Mkata iliyopo halmashauri ya Tanga Vijijini kutekeleza kwa vitendo  agizo lililotolewa na Waziri wa Maji Juma Aweso la kutaka kuimaliza kero na changamoto ya maji ambayo inawakumba wakazi wa eneo hilo.

Aweso alitoa agizo hilo  
 wakati wa ziara ya kikazi ya  Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM)  Taifa,  Paul Makonda ambapo msafara wake  uliposimama katika eneo hilo la Msata   ukitokea Mkoani Pwani na kuagiza  huduma ya maji safi na salama iwafikie wananchi hao.
Akizungumza mara baada ya kuwasili katika eneo hilo ikiwa ni katika kutekeleza maagizo hayo ya Waziri Kaimu mtendaji huyo wa Dawasa  Kiula alisema kwamba  kwa sasa wakazi wa eneo hilo la Msata wanapata maji ambayo sio toshelevu kutoka na kuwepo kwa ongezeko kubwa la idadi  ya wananchi.

"Kimsingi tumefika katika eneo hili la Msata mashariki na hii ni hii tunatekeleza wito na maagizo ambayo yametolewa na Waziri wa maji Juma aweso kwa hivyo tumefika ili kuitatua changamoto hii ya maji,"alisema Kingu.


Kingu alibainisha kwamba katika eneo hilo sio kwamba halina huduma ya maji safi na salama isipokuwa maji yaliyipo kwa sasa hayawezi kutosheleza kutoka na kuwa na ongezeko kubwa la wakazi ambao wanafikia zaodi ya elfu 90.

 Aidha aliongeza kuwa mipango ambayo inafanyika kwa sasa na  Dawasa ni kufanya jitihada za haraka katika  kupeleka huduma ya maji kupitia chanzo cha maji kilichopo kutoka  tenki la maji lililopo kijiji cha Manga. 

Pia alibainisha  kuwa sambamba na kuongeza wingi wa maji pia Mamlaka itahakikidha  itaboresha  miundombinu yote ya maji ambayo ipo katika kata ya Mkata ili iweze kuhudumia wananchi kwa urahisi.

"Ukiangalia eneo hili la mkata wakazi wanazidi kuongezeka zaidi ukilinganisha na siku za nyuma hivyo ni lazima tuweke mipango ya kuboresha miundombinu ya maji na kuvuta maji kutoka maeneo ya jirani na hii itasaidia sana kwa wananchi kupata maji ya uhakika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Mkata Mashariki , Zamini Kafuluma ameupongeza uongozi wa   DAWASA kwa kufika katika eneo hilo kwa lengo la kujionea na kutekeleza maagizo ambayo yametolewa na Waziri wa Maji pamoja na Katibu wa Itikadi na uenezi wa Chama cha mapinduzi (CCM) Taifa.
Mwenyekiti huyo aliongeza kitendo walichokifanya Dawasa ni kutekeleza Ilani ya chama kwa vitendo kwa lengo la kuhakikisha wanasogeza huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi.

Siku chache zilizopita Katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha Mapinduzi ,(CCM) Taifa Paul Makonda alipokuwa katika ziara yake ya kikazi akiwa na Waziri wa Maji Juma Aweso walitoa maagizo kwa uongozi wa Dawasa kufika katika eneo la Msata mashariki ili kutatua ya maji kwa wananchi jambo ambalo limeanza kutekelezwa  kwa vitendo na  Dawasa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.