Mwenyekiti wa Vijana KKKT (KDMs) Usharika wa Makorora Jimbo la Pwani Steven Mduma amewataka wahitimu Chuo cha Afya –Bombo kuzingatia upendo na uaminifu kufikia malengo yao waliojiwekea.
Mduma aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa akizungumza katika mahafali ya Umoja wa Wanafunzi Wakristo katika chuo hicho ambapo alisema kwamba hayo ndio mambo muhimu ya msingi ya kuzingatia baada ya kumaliza chuo ili waweze kufikia ndoto zao walizojiwekea wanapokuwa kazini.
Mduma aliwataka pia wahitimu hao kujiepusha na vitendo vya rushwa kwani vinakwamisha juhudi za kimaendeleo na kupelekea kushindwa kutimiza malengo yao hivyo wahakikishe wanaachana navyo.
“Ndugu zangu leo hii mnatarajiwa kumaliza hapa chuoni na kwenda kwa jamii hivyo niwaase mhakikishe mnakwenda kuishi kwa, uaminifu, upendo mkiwa kama vijana leo mnahitimu kutoka hatua moja kwenda nyengine”Alisema
Hata hivyo aliwataka pia wanaohitimu kwenda kufanya kazi kwa ujasiri, nguvu na uaminifu ambao utakuwa chachu yao kuweza kufikia mafanikio.
Aidha katika Halfa hiyo Mwenyekiti huyo alihaidi kutoa laki tano kwa ajili ya kuchangia vyombo vya mziki na kutunisha mfuko wa umoja huo ili kuhakikisha wanapiga hatua ,kubwa za kimaendeleo
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.