Na Victor Masangu,Kibaha
Baraza la madiwani Halmashauri ya mji Kibaha limeazimia kwa pamoja kumpongeza kwa dhati serikali ya awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia kiasi cha shilingi bilioni 8.1 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2022/2023.
Akisoma taarifa ya mapokezi na matumizi ya fedha ya mwaka wa fedha 2022/2023 kutoka serikali kuu Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Kibaha Mussa Ndomba amebainisha kuwa fedha hizo zitakwenda kutekekeza miradi mbali mbali ya maendeleo ambayo itasaidia kusogeza huduma kwa wananchi.
Ndomba alibainisha kwamba katika fedha hizo walizopatiwa zitakwenda kuleta chachu ya maendeleo hususan katika sekta ya elimu,afya,maji,utawala,nishati ya umeme,miundombinu ya barabara,pamoja na suala la uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia asilimia 10 ya makusanyo ya mapato ya ndani.
"Kwa Upande wa halmashauri ya mji kibaha kupitia Ofisi ya mkurugenzi tunamshukuru Sana Rais wetu kutupatia hizi fedha kwa kipindi hiki cha mwaka 2022/2023 kiasi cha zaidi ya bilioni 8.1 hii ni sawa na asilimia 100 kutoka vyanzo mbali mbali.
Mwenyekiti huyo alibainisha kuwa vyanzo hivyo ni kutoka serikalini kuu, kiasi cha shilingi bilioni 1,969,958,103,.91 fedha kutoka kwa wahisani na wadau wa maendeleo ni bilioni 2.5,fedha zilizotolewa nje ya bajeti ni bilioni 2.2 huku fedha za mapato ya ndani ni shilingi bilioni 1.4.
Kadhalika alifafanua kuwa kwa Upande wa nishati ya umeme imeendelea kuwa vizuri kutokana na kutekelezwa kwa miradi mikubwa miwili katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 ambayo itaweza kusaidia upatikanaji wa nishati ya umeme kwa wananchi ambao walikuwa wana changamoto hiyo.
Kuhusiana na uboreshaji wa miundombinu ya barabara kupitia Tarura halmashauri hiyo ina mtandao jumla ya kilometa 504.27 ambapo kati ya hizo kilometa zipatazo 25.33 ni lami,kilometa 89.70 ni changarawe,huku kilometa 389.24 zipo katika hali ya udongo.
Akifafanua kuhusiana Tanroad mtandao wa barabara kuu zinazosimamiwa na Mkoa zina urefu wa kilometa 503.66 ambazo zote ni kiwango cha lami huku barabara nyingine za Mkoa zina jumla ya kilometa 875.75 ambazo zimejumuisha kilometa 49.71 za tabaka la lami na kilometa 826.30 udongo wa changarawe na udongo.
Aidha Baraza hilo la madiwani limetoa ombi maalumu kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuiwezesha halmashauri ya mji Kibaha kupandishwa adhi na kuwa manispaa kutokana na kuwa makao makuu ya Mkoa wa Pwani.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nikson Saimon amewataka madiwani hao kuhakikisha wanawatumikia wananchi wao ikiwa sambamba na kuweza kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo katika sekta tofauti.
Pia alilihimiza baraza hilo la .madiwani kutunga sheria ndogo ndogo usheria ndogo ndogo ambazo zitaweza kuwa rafiki zaidi kwa wafanyabiashara wadogo ili wasiwe na vikwazo vyovyote katika utekelezaji wa kujipatia kipato.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.