Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shillow akizungumza wakati wa mafunzo kwa vijana kuhusu fursa za uvuvi huku akitoa wito ametoa wito kwa vijana kutumia fursa za uwepo wa bahari katika Jiji hilo ili kuweza kujikita kwenye uvuvi wa kisasa ambao utawawezesha kuweza kujikwamua kiuchumi wao na jamii zaio
Mwakilishi wa Shirika la Botnar Foundation Philotheusy Mbogoro ambayo inatekeleza mradi wa Tanga Yetu ndani ya Jiji la Tanga akielezea malengo yao ni kuhakikisha mpaka kufikia mwaka 2030 vijana na ndani ya Jiji la Tanga wawe wamejikwamua kiuchumi.
Aunt Sadaka akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo |
Aunt Sadaka akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mafunzo hayo
Sehemu ya washiriki wa kikao hicho
Na Oscar Assenga,TANGA.
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shillow amefungua mafunzo kwa vijana kuhusu fursa za uvuvi huku akitoa wito ametoa wito kwa vijana kutumia fursa za uwepo wa bahari katika Jiji hilo ili kuweza kujikita kwenye uvuvi wa kisasa ambao utawawezesha kuweza kujikwamua kiuchumi wao na jamii zao.
Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa mafunzo kwa vijana kuhusu fursa za uvuvi yaliyoandaliwa na Shirika la Botnar Foundation yakilenga kuhakikisha wanatumia fursa za uwepo wa rasimali bahari vema ili kuweza kunufaika nayo.
Shillow alisema amesema kwamba kumekuwa na wimbi kubwa la vijana kutopenda kufanya hali inayowapelekea kujiingiza kwenye shughuli zisizofaa hivyo ni vema wakaona namna ya kubadilisha mitazamo yao kwa kujikita kwenye fursa za uvuvi ambazo zitawezesha kuinua vipato vyao.
Awali akizungumza wakati wa Mafunzo hayo Mwakilishi wa Shirika la Botnar Foundation Philotheusy Mbogoro ambayo inatekeleza mradi wa Tanga Yetu ndani ya Jiji la Tanga alisema malengo yao ni kuhakikisha mpaka kufikia mwaka 2030 vijana na ndani ya Jiji la Tanga wawe wamejikwamua kiuchumi.
Alisema kwamba hatua hiyo inatokana na uwepo wa fursa mbalimbali ambazo vijana wakizitumia vizuri zinaweze kuwasaidia kunufaika na hivyo kuweze kujikwamua kiuchumia wao na jamii zao zinazowazunguka.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Dkt Sipora Liana alisema kwamba wametenga jumla ya ekari 200 kwa matumiziya kilimo kwa vijana ikiwa ni jitihada za kutoa ajira kwa kundi hilo.
Alisema tayari imeshatenga eneo hilo la kilimo na kwamba vijana wanatakiwa kujiunga katika vikundi vyenye usajili ambavyo vitapewamikopo ya kuanzishia shughuli hizo.
“Hii ni fursa nyingine kwa vijana wa Tanga,changamkieni fursa hii ili muweze kunufaika badala ya kulalamika kila siku kwamba hakuna ajira...mtazalisha mazao mbalimbali chini ya usimamizi wa maafisa wetu ugani ambao watawasaidia pia kupata masoko”alisema Liana.
Alisema kupitia mradi wa Tanga yetu kwa kushirikiana na Halmashauri na Botna vijana wameweza kujengewa uwezo wa uelewa wa uzalishaji na namna ya kutumia mikopo inayotolewa kupitia mapato ya ndani ya Jiji la Tanga.
Naye kwa upande wake mmoja wa washiriki wa Mafunzo hayo Abdallah Mohammed mkazi wa Kisosora ni mmoja walionufaika na mafunzo hayo alisema kwamba yatakavyowasaidia kuweza kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Abdallah alitoa wito kwa vijana kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii ili kujiepusha dhidi ya vitendo visivyofaa ambavyo vinaweza kuwarudisha nyuma kimaendeleo
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.