Na Victor Masangu,Kibaha.
Mke wa mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Selina Koka ameahidi kuwainua kiuchumi wanawake wa kata ya misugusugu na kongowe kwa kuwawezesha kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali pamoja na kuwapatia mitaji ya fedha ili kuondokana na umasikini.
Selina ambaye pia ni mlezi wa UWT Wilaya ya Kibaha mji amesema lengo lake kubwa kuwapambania wanawake wote was uwt kwenye Jimbo la Kibaha kwa kuwasaidia waweze kufanikiwa katika shuguli zao mbali mbali za ujasiriamali.
"Ninachotaka kukifanya ni kuwawezesha wanawake wajasiriamali ili waweze kuanzisha biashara zao ambazo zitawasaidia kujipatia fedha na kujikwamua kiuchumi na kwamba nitasaidia katika kata zote 14 za Jimbo hili,"alisema Mgonja.
Alifafanua zaidi Selina Koka aliongeza kuwa mikakati yake ni kuwafungulia akaunti wanawake wa UWT kwa kuwapa kiasi cha shilingi laki tano ili waweze kuanzisha biashara.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha mji Elina Mgonja amebainisha kwa kwa sasa katika kata ya misugusugu kumekuwa na maendeleo katika sekta mbali mbali.
Aliongeza kuwa Mbunge Koka amekuwa mstari wa mbele katika kusikiliza kero na changamoto mbali mbali zinazowakali na kuzifanyia kazi katika maeneo ya afya,elimu pamoja na miundombinu ya barabara.
"Kitu kitubwa sisi wanawake inabidi tuachane kabisa na mambo ya makando kando na kuwahimiza watu kulipa ada kwa wakati lengo ikiwa ni kujizatiti katika kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa,"alisema Mgonja.
Katika hatua nyingine alimpongeza kwa dhati mlezi wa UWT Selina Mgonja kwa juhudi zake za kusaidia wanawake katika kuwawezesha ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kwamba ziara yake ni kuangalia uhai wa chama.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.