NA ALBERT G.SENGO/MWANZA
Yesu aliubeba msalaba, ingawa ulikuwa mzito na ulimchosha alipambana nao mpaka mwisho na kuishinda mauti na hata leo hii ndiye mkombozi wetu. Tutoke kwenye msalaba wa Goligota twende kwenye msalaba wa kijamii, tunapotafuta shortcut/njia za mkato kujinufaisha tukaingia kwenye ufisadi na dhuluma, tumeukwepa msalaba/majukumu tuliyo kabidhiwa. - Ukiwa na nidhamu ya kuamka mapema na kuwahi kazini, umeamua kuubeba msalaba, - Kama wewe ni baba au mama ukiishi kwa kutimiza majukumu yako, kwa watoto kupata elimu, chakula na malazi safi na salama, umeamua kuubeba msalaba. - Kama wewe ni mwanasheria, daktari au muuguzi na umeamua kufanya kazi kwa misingi ya taaluma yako kuwaokoa wagonjwa na wenye tabu na shida, umeamua kuubeba msalaba. - Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa siku za hivi karibuni amekuwa akipokea ripoti ya CAG yenye hati nyingi chafu, humo ndani watu wamepiga hela nyingi mabilioni kwa mabilioni ya fedha, mpaka rais anatumia lugha kali yenye ukakasi, yote yamesababishwa na watendaji aliowaamini na kuwapa majukumu kusimamia anachokipambania kwa maslahi ya taifa lakini wao wameamua kumwangusha kwa kufanya kwa njia zao, kwa maslahi yao, kwa ufupi wameukwepa msalaba. Yesu amefanya kitu ambacho sayansi haiwezi kufanya. - Yeye alivunja miiko ya sayansi. Ni sehemu ya ufafanuzi kwa swali, nililomuuliza Padre Leons Maziku, Muhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Mtakatifu Agustino Mwanza Tanzania (SAUT) swali likiwa - Kuna lipi la kujifunza kwa jamii yetu kupitia Pasaka na mateso ya Bwana Yesu Kristu pale msalabani?Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.