NA ALBERT G. SENGO
Kifo cha msanii aliyeshinda tuzo nyingi Costa Titch, kwa jina halisi Constantinos Tsobanoglou, kimeibua mshtuko mkubwa siyo tu nchini Afrika ya kusini lakini pia wapenzi wa muziki wake dunia kote. Rapa huyo alifariki siku ya Jumamosi kuamkia Jumapili ya leo baada ya kuanguka jukwaani wakati wa onyesho kwenye tamasha la muziki la Ultra SA, lililofanyika katika ukumbi wa Expo Centre mjini Nasrec, Johannesburg. Alikuwa akitumbuiza katika Chumba kipya cha Smirnoff Storm, ambacho kilikuwa jukwaa la wapenzi wa muziki wa amapiano na afro-tech. Alianguka mara mbili jukwaani kabla ya kutolewa nje ili kupokea matibabu. Familia yake ilithibitisha juu ya kifo chake mapema hii leo asubuhi katika taarifa ya vyombo vya habari, iliyotolewa kwenye mitandao yake ya kijamii. Wamethibitisha kuwa alikuwa na umri wa miaka 28, wakati wa kuaga kwake. #costatitch #RiPcostaTitch #Costa #TitchTupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.