ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, February 12, 2023

HATIMAYE MELI YA KITALII YA KWANZA TANZANIA MV MWANZA HAPA KAZI TU YAANZA MAJARIBIO ZIWA VICTORIA

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Hatimaye Serikali imefanikiwa kuishusha majini meli mpya itakayokuwa ni kubwa kuliko zote ndani ya Victoria ya Mv.Mwanza “Hapa kazi tu” baada ya ujenzi wake kukamilika kwa hatua ya pili ya asilimia 82. Meli hiyo yenye urefu wa mita 92.6, kimo cha mita 20 na upana wa mita 17 imeshushwa leo February 12, 2023 ikiwa ni miaka minne tangu ilivyoanza kujengwa Januari 2019 jijini Mwanza. Hadi kukamilika kwake, meli hiyo itakuwa na uzito wa tani 3,500 ikiwa ni ongezeko la tani 500 zaidi kutoka tani 3,000 zilizorekodiwa leo wakati ikishushwa majini ndani ya Ziwa Victoria. Baada ya kukamilika na kuanza safari, meli hiyo itakuwa kubwa kuliko zote katika Ziwa Victoria. Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya huduma za meli nchini (MSCL) Erick Hamis ameeleza leo baada ya zoezi la ushushaji wa meli hiyo kukamilika kuwa kilichofanyika ni hatua muhimu ya pili katika ujenzi wa meli hiyo. Amesema sehemu kubwa ya ujenzi wa meli hiyo imefanywa na Watanzania kwa asilimia 100 wenye umri wa kati ya miaka 21 hadi 35 ambao walishirikiana na wakandarasi sita (6) kutoka nje ya nchi.

‘Bado kidogo ikamilike’ Hamis amesema hatua ya tatu ya ujenzi huo itakuwa ni kufanya majaribio, kupaka rangi kuweka vifaa vya kuongozea meli, kazi ambayo itadumu kwa muda wa kati ya miezi mine hadi mitano. "Mpaka hapa ilipofikia tunaweza kusema meli imekamilika na hiyo asilimia 18 iliyobaki ni ukamilishaji wa mambo madogomadogo tu ambayo yatafanyika kwa kipindi kisichopungua miezi minne," amesema Hamis. Ujenzi wa meli hiyo unatarajiwa kugharimu zaidi ya Sh109 bilioni kupitia fedha za walipa kodi. "Mpaka sasa mkandarasi amelipwa zaidi ya bilioni 93.8 na kwa sasa serikali ndiyo inamdai kazi na atakapoikamilisha kiasi kilichobaki atapatiwa,” amesema Hamis. Baada ya meli hiyo kukamilika, bosi huyo amesema wataalamu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (Tasac) watakagua na kutoa chetu cha ubora na itakuwa kifanya safari zake kati ya Bandari za Bukoba, Kemondi, Jinja na Portbell nchini Uganda, Kisumu nchini Kenya, Musoma na Mwanza.
#mwanza #samiasuluhuhassan #ikulumawasiliano #bungenidodoma #lakevictoria #dodoma #kaziiendelee #hapakazitu

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.