Sisi Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi, CCM (UWT) tumepokea kwa furaha kubwa kitendo cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kumtunuku Shahada ya Udaktari wa Heshima Rais na Mwenyekiti wa Chama chetu cha Mapinduzi, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.
Umoja wetu wa UWT tunampongeza Dkt Samia tukitambua juhudi zake zisizomithilika za kuleta maendeleo maridhawa nchini katika muda mfupi wa miaka miwili Ikulu.
Mwenyekiti wetu Dkt Samia, kama ambavyo amekuja na Falsafa yake ya (4R) ya uongozi bora; Reconciliation (Maridhiano), Resiliency (Ustahamilivu), Reforms (Mabadiliko) na Rebuilding (Kujenga Upya), ameleta Mapinduzi makubwa katika kila Sekta nchini na hivyo anastahili kupongezwa.
Ni dhahiri sasa kupitia falsafa hii ameirejesha Nchi katika uimara wake kiuchumi, kisiasa na kijamii tukizingatia ameipokea Nchi yetu katika wakati mgumu wa kuondokewa ghafla na Mtangulizi wake Rais Magufuli, gonjwa la Corona na Vita ya Urusi na Ukraine ambavyo kwa pamoja vimesababisha kushuka kwa uchumi si Tanzania pekee bali pia dunia kote.
Leo hii mahusiano ya Kitaifa na Kimataifa, Diplomasia ya kiuchumi, Haki za Binadamu, Demokrasia ya vyama vingi, Maendeleo ya watu, Umoja wa Kitaifa, Utu, amani, Usalama na Ulinzi wa wananchi na Nchi, Maslahi ya makundi yote nchini; wakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara ni baadhi ya vitu vilivyoboreshwa kwa kiwango kikubwa ndani ya miaka miwili tu ya Dkt Samia madarakani.
Dkt Samia kama Mwanamke wa kwanza kuwa Rais wa Tanzania tangu tupate Uhuru mwaka 1961, kupitia Uongozi wake makini ameithibitishia Tanzania na dunia kwamba kwa hakika Mwanamke akipewa nafasi anaweza. UWT tunajivunia sana Kiongozi wetu huyu mwanamke.
UWT tunaziomba Taasisi zote duniani zenye hadhi ya kutoa tuzo zimpatie tuzo za heshima Rais wetu bila kusita kwani ana kila sababu na hadhi hiyo.
Mwisho UWT tunawaomba WaTanzania wote waendelee kumpa ushirikiano wa kutosha Rais wetu Dkt Samia ili aendelee kutuletea maendeleo lukuki WaTanzania wote na kupata moyo wa kuendelea kuiheshimisha Nchi yetu duniani.
Imetolewa na:
MCC Mary Pius Chatanda,
Mwenyekiti wa UWT Taifa.
Novemba 30, 2022.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.