Na Victor Masangu,Pwani
Katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta ya afya Mamlaka ya mapato (TRA) Mkoa wa Pwani imetoa msaada wa vifaa tiba katika kituo cha afya mlandizi kilichopo Kibaha Pwank kwa lengo la kuboresha huduma hususan kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Hayo yamebainishwa na meneja wa TRA Mkoa wa Pwani Emmanuel Maro wakati wa halfa fupj ya kukabidhi vifaa hivyo ikiwa ni wiki ya mlipa Kodi katika ngazi ya mkoa ambapo pia wameweza kutoa msaada mingine katika vituo viwili vya watoto yatima vilivyopo Wilayani Kibaha ikiwa ni mchango katika jamii.
Meneja huyo alisema kwamba wamekwenda kutoa msaada wa vifaa tiba mbali mbali katika kituo hicho kutokana na kubaini kuwepo kwa uhitaji zaidi kwa watoto wadogo wenye umri chini ya miaka mitano lengo ikiwa ni kuboresha sekta ya afya hasa kwa watoto.
Pia alifafanua kwamba katika kilele cha kuadhimisha wiki ya mlipa kodi kutafanyika kongamano ambalo litaambatana na utoaji wa tuzo mbali mbali kwa washindi ambao wameweza kufanya vizuri katika makundi madogo ya Kati pamoja na yale makundi makubwa na waliochangia bila shuluti.
"Katika wiki hii ya mlipa kodi sisi Kama TRA Mkoa wa Pwani tumeweza kufanya shughuli mbali mbali za kijamii ambapo tumewatembelea wafanyabiashara mbali mbali ikiwa pamoja na kutoa elimu na kutoa shukrani kwa kwa kipindi Cha mwaka mzima,"alisema Maro.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibaha amewataka wafanyabiashara wote kuanzia ngazi za chini,kati na wale wakubwa kuhakikisha wanalipa kodi zao kwa mujibu wa kanuni sheria bila kukwepa kwa lengo la kuliletea Taifa maendeleo.
Aidha mkuu huyo aliwapongeza TRA kwa kuona umuhimu mkubwa wa kuamua kuwatembelelea wafanyabiashara mbali mbali wa Mkoa wa Pwani na kuwapatia elimu juu umuhimu wa kulipa kodi pamoja na kutoa shukrani zao.
Naye mganga mfawidhi wa kituo Cha afya mlandizi ameishukuru TRA kwa kuona umuhimu wa kutoa vifaa tiba hivyo ambavyo vitakuwa ni mkombozi mkubwa katika kuwasadia kuokoa maisha ya watoto ambao walikuwa na shida ya kupumua.
Naye mmoja wa waanzilishi wa vituo cha watoto yatima cha karibu nyumbani kilichopo wilayani Kibaha ameishukuru kwa dhati TRA kutumia wiki ya mlipa kodi kwenda kutoa msaada wa vifaa mbali mbali kwa ajili ya mahitaji ya watoto.
Katika wiki ya mlipa kodi TRA Mkoa wa Pwani imeweza kufanya shughuli mbali mbali ikiwemo kutoa msaada kwa vituo viwili vya kulea watoto yatima, pia wametoa vifaa tiba katika kituo cha afya mlandizi pamoja na kutoa shukrani na elimu kwa mlipa kodi mlango kwa mlango kwa kuwafata wafanyabiashara katika maeneo yao ya biashara.
Kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho ya wiki ya mlipa kodi inasema asante kwa kulipa Kodi kwa ustawi wa jamii na maendeleo ya nchi yetu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.