Matukio katika picha ibada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu Mkuu Mussa Masanja Magwesela pamoja na Makamu wake Zakayo E Bugota wa kanisa African Inland Church Tanzania (AICT) tarehe 06.11.2022 Makao makuu ya kanisa Ushirika wa AICT Makongoro. Ibada huyo ya kuwekwa Wakfu imeongozwa na Askofu Mkuu Mstaafu Charles Shilangi Salalah na mahubiri yaliyotolewa na Askofu Mkuu Mstaafu AIC Kenya Rev Dkt Silas Yego.
Mgeni rasmi katika ibada hiyo upande wa serikali alikuwa ni Mhe Dotto Biteko Waziri wa Madini, Mary Masanja Naibu Waziri Maliasili na utalii ambaye pia Mbunge Viti Maalum akiwakilisha mkoa wa Mwanza, Mhe Constantine Kanyasu Mbunge Geita Mjini, Mkuu wa Wilaya ya Geita akiongozwa na Mkuu wa Wilaya Mwenyeji Hassan Masala aliyemwakikisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Wawakikishi wa Mbunge Jimbo la Nyamagana Bi Florah Magabe na Badlina Mpangalala.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.