Mshambuliaji matata Cristiano Ronaldo ametimuliwa na klabu ya Manchester United baada ya uhusiano wake na miamba hao wa Uingereza kusambaratika kabisa. Cristiano Ronaldo (kulia) na kocha wa Manchester United Erik ten Hag.
Kwa mujibu wa Manchester United, nyota huyo anaondoka klabuni humo mara moja baada ya kuafikiana makubaliano ya kuhimitisha ndoa yao kwa mara ya pili.
"Cristiano Ronaldo anaondoka katika klabu ya Manchester United mara moja baada ya kuafikiwa kwa makubaliano baina ya pande zote.
Klabu hii inamshukuru kwa mchango wake mkubwa katika vipindi viwili ambavyo amehudumu Old Trafford," United imesema kupitia kwa taarifa.
Ronaldo anaondoka miezi 15 tu baada ya kurejea Old Trafford Ronaldo alirejea Manchester United Agosti mwaka 2021 miaka 13 baada ya kuondoka akielekea Real Madrid ambako alidumu kwa miaka tisa na kushinda mataji mengi kabla ya kutia Juventus ya Italia.
Baada ya kurejea mwaka jana, Ronaldo anaondoka Manchester United akiwa amefunga jumla ya mabao 145 katika mechi 364 ambayo amechezea miamba hao wa Uingereza katika mihula miwili.
Kusambaratika kwa ndoa ya Ronaldo na Manchester United Uhusiano wa United na Ronaldo ulisambaratika kabisa wiki jana baada ya nahodha huyo wa Ureno kuilima vikali klabu hiyo katika mahojiano na mwanahabari Piers Morgan.
Ronaldo aliwasuta wamiliki wa United - Glaziers, kumsuta kocha mkuu Erik Ten Hag akidai kusalitiwa na kukosewa heshima katika klabu hiyo.
Mwenendo wa Ronaldo ulikisiwa kusababisha msukosuko klabuni humo na baada ya kumtimua, United inasema kuwa timu hiyo inalenga kuendelea kupiga hatua ya pamoja chini ya Ten Hag.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.