Chama cha Wasiomuamini Mungu Nchini, (AIK) kinadaiwa kufilisika kiasi cha kushindwa kugharamikia shughuli zao za kila siku.
Akiandika ujumbe kwenye Twitter siku ya Jumatatu, Novemba 7, chama hicho kimewaomba wasamaria wema kuwasaidia kulipa kodi ya afisi ya KSh 18,000 kila mwezi.
Pia, kwa ushirikiano na Shirika la Haki za Kibinadamu la chama hicho, kinaendeleza kampeni inayolenga kuchangisha pesa za kumsaidia kiongozi wao Harrison Mumia. "Pesa hizo zitamsaidia kiongozi Harrison Mumia, kugharamikia kodi akiwa anafanya kazi baada ya kufutwa kazi aliokuwa- ndiposa aweze kumakinina na kazi yake ya kuongoza chama hicho cha kipkee kisichomuamini Mungu kilichosajiliwa Kenya," taarifa hiyo ilisoma.
Chama hicho pia kimesema pesa zitakazochangwa zitasaidia kufadhili kesi kortini, kikisema kimekuwa kikipigwa vita na mashirika mengine ya kidini na wanachama wa serikali ya Kenya.
"AIK inashabuliwa na wanachama wa serikali ya Kenya ambao wanataka kuharamisha shirika hili la wasimoumini Mungu na kuenda kinyume na haki yao ya kikatiba inayotambulika kwenye vifungu vya sheria nambari 32 na 36,"
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.