ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 6, 2022

WIZARA YA ELIMU YAIBAMIZA WIZARA YA SHERIA NA KATIBA KWA SETI 32-8 MICHUANO SHIMIWI TANGA

 

Mchezaji wa mchezo wa Pete wa timu ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia wenye jezi za zambarai   kushoto akiwania mpira dhidi ya wa Wizara ya Sheria na Katiba wakati wa mechi ya Mchezo wa Pete katika michuano ya Shimiwi yanayoendelea kwenye viwanja vya Bandari Jijini Tanga ambapo katika mchezo huo Wizara ya Elimu iliibuka na ushindi wa seti 32-8
Mchezaji wa timu ya Pete wa Wizara ya Wizara ya Sheria na Katiba akiwania mpira  dhidi ya wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia  wakati wa mechi ya Mchezo wa Pete katika michuano ya Shimiwi yanayoendelea kwenye viwanja vya Bandari Jijini Tanga ambapo katika mchezo huo Wizara ya Elimu iliibuka na ushindi wa seti 32-8 
Mchezaji wa mchezo wa Netbali wa timu ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia wenye jezi za zambarai  akijiandaa kufunga bao wakati wa mechi dhidi ya wa Wizara ya Sheria na Katiba katika michuano ya Shimiwi inayoendelea kwenye viwanja vya Bandari Jijini Tanga ambapo katika mchezo huo Wizara ya Elimu iliibuka na ushindi wa seti 32-8
Mchezaji wa mchezo wa Netbali wa timu ya Wizara ya Sheria na Katiba kushoto akifunga moja ya bao la timu hiyo dhidi ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika michuano ya Shimiwi inayoendelea kwenye viwanja vya Bandari Jijini Tanga ambapo katika mchezo huo Wizara ya Elimu iliibuka na ushindi wa seti 32-8


 Na Oscar Assenga,Tanga


TIMU ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imeibamiza Wizara ya Sheria n Katiba kwa kuwafunga seti 32-8 katika mchezo wa mpira wa Pete uliofanyika kwenye viwanja vya Bandari Jijini Tanga.

Katika mchezo huo ambao Wizara ya Elimu ikiutawala mchezo huo kwa asilimia kubwa ambapo kila walipokuwa wakipata nafasi ya kufungua wafungaji wao walikuwa wakiweka langoni mabao hayo.

Mpaka timu hizo zinamaliza mzunguko wa kwanza timu ya Wizara  Elimu ilikuwa ikiongoza kwa kuwafunga wapinzani wao Wizara ya Sheria na Katiba seti 19 kwa 2.

Wachezaji wa timu ya Wizara ya Elimu walionekana mahiri kwa kucheza vema huku wakicheza pasi nzuri ambazo ziliwawezesha kuweza kutawala mchezo huo huku wakishangiliwa na umati mkubwa wa wanamichezo waliofurika kushuhudia mchezo huo.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo Meneja wa timu hiyo Moshi Saidi alisema kwamba ushindi huo ni Salama tosha kwa timu ambazo watakutana nazo kwenye michezo mengine na kwamba wamehaidi kuendeleza wimbi la ushindi.

"Kama unavyojua sisi tumekuja kushiriki mashindano haya na tunamatumaini makubwa ya kuny'akua vikombe vyote na tumejipanga kikamilifu kuweza kupambana na kutImiza lengo letu"Alisema

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.